Tuesday 12 December 2023

TIA kampasi ya singida yaendesha zoezi la uchangiaji ya Waathirika wa mafuriko Hanang.

 
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imeendesha zoezi la uchangiaji  kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh, wilayani Hanang mkoani Manyara.

Ambapo zoezi hilo limeenda sambamba na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake.

Kampeni hii huwafanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika kuanzia tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili yakupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.

PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON, DOTTO MWAIBALE-SINGIDA.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Bi. Flora Lemunge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Desemba 9, 2023 katika viwanja vya taasisi hiyo wakati wa zoezi la uchangiaji kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh, wilayani Hanang mkoani Manyara.

Jeshi la polisi Singida pamoja na wananchi,wasanii waliojitokeza katika zoezi hilo wakichangia damu kwaajili ya waathirika wa mafuriko.
Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakiendele kuosha magari. 
Wanafunzi wa  Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakitoa burudani wakati wa zoezi hilo. 
Msanii wa Bongo Fleva H. Kelly Lamata akiwa pamoja na msanii mwingine wakitoa burudani kama mchango wao.

Michezo ikiendelea kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida.

Sunday 10 December 2023

Serikali yatoa mil. 114/- kituo Cha Afya Mtae, MSD yakikabidhi vifaa tiba

Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Mary Isango, akimpatia nyaraka mbalimbali, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtae kilichopo Lushoto mkoani Tanga, Shafii Makamba (kulia), wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.Milioni 114 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kununulia vifaa hivyo kupitia MSD kwenye tukio la makabidhiano lililofanyika Disemba 9, 2023. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Dereva wa MSD, Rashidi Msambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtae, Andrew Kilama. 

.........................................................

Na Dotto Mwaibale, Lushoto

SERIKALI imetoa Sh.Milioni 114 kwa Kituo cha Afya  Mtae kilichopo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambazo zimetumika kununulia vifaa tiba kupitia Bohari ya Dawa (MSD) na hivyo kinatarajia kuanza kutoa huduma ya upasuaji mwishoni mwa mwezi Disemba 2023.

Hatua ya kituo hicho kuanza  kutoa huduma hiyo inatokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya kuibadilisha zahanati ya kijiji cha Mtae kuwa Kituo cha  Afya ili wananchi waweze kupata huduma bora na karibu.

Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,  Shafii Makamba akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo kutoka MSD alianza kwa kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani kupitia MSD kwa kuwezesha kutoa vifaa hivyo vya dharura kwa ajili ya kufanya huduma ya dharura kwa wakina mama na watoto.

"Vifaa hivi tulivyovipokea leo kutoka MSD Kanda ya Tanga  vitasaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kwa sababu kabla ya hapo walikuwa wakilazimika kutembea umbali usiopungua kilometa 65 kwenda Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kupata huduma za dharura hasa za upasuaji na kuwa wataachana na adha hiyo na kupata huduma hii hapa hapa katika kituo chetu," alisema Makamba.

Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Tanga, Mary Isango akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Meneja wa MSD wa kanda hiyo, Sitti Abdulrahman, alisema wamepeleka vifaa hivyo baada ya kituo hicho cha afya kujengwa jengo la upasuaji na kupelekewa vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh.Milioni 114 ambavyo vinaenda kuondoa changamoto waliyokuwa wakiipata wananchi kwenda kupata huduma hiyo mbali.

"Huduma za upasuaji sasa zitafanyika katika kituo hiki baada ya kupata vifaa hivi ambavyo ni muhimu sana sisi kama bohari ya dawa wito wetu kwa watendaji wa kituo hiki ni kuvitunza ili viweze kudumu muda mrefu na kuleta tija kwa wananchi kadri watakavyokuwa wakiendelea kuvitumia kwa kuzingatia kuwa Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuvinunua," alisema Isango.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mtae, Beatrice Alphonce, Disifa Mdoe na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Andrew Kilama waliishukuru Serikali kupitia MSD kwa kuwapelekea vifaa hivyo ambavyo vitaondoa kabisa madhira waliyokuwa wakiyapata na wakati mwingine kusababisha vifo.

"Tulikuwa na changamoto kubwa baadhi ya wajawazito walikuwa wakijifungulia njiani kutokana na umbali mrefu wa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kupata huduma lakini sasa tutakuwa tunaipata hapahapa nyumbani kwa kweli tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu mama Samia kwa kutuona na kutuonea huruma wanawake wenzake na kama ingewezekana tungemuomba siku moja aje hayaone kwa macho maendeleo haya aliyotuletea," alisema Alphonce.

Alphonce alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia, Mbunge wa jimbo hilo, Rashid Shangazi na viongozi wa wilaya hiyo kwa jitihada kubwa wanayoifanya ya kuwaletea maendeleo hayo ambapo aliwaombea kwa Mungu awape afya na maisha marefu.Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Mary Isango na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtae, Shafii Makamba wakizipitia nyaraka hizo kabla ya kukabidhiana vifaa hivyo.Mapitio ya nyaraka hizo yakifanyika kwa pamoja kabla ya makabidhiano. Kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Mary Isango, Dereva wa MSD, Rashidi Msambo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtae, Andrew Kilama na  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtae, Shafii Makamba,Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtae, Andrew Kilama akishukuru Serikali kwa kuwapelekea vifaa hivyo kupitia MSD,Muonekano wa Zahanati ya Kijiji cha Mtae kabla ya kubadilishwa kuwa Kituo cha AfyaMuonekano wa jengo la upasuaji lililojengwa na Serikali na kuipandisha adhi zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya.Vifaa tiba hivyo vikitolewa kwenye gari tayari kwa makabidhiano.Vifaa tiba vikipelekwa kwenye jengo la upasuaji.Watoto wa Kijiji hicho wakishiriki kubeba vifaa hivyo.Kazi ya ubebaji wa vifaa hivyo ikiendelea.Vifaa vikibebwa.Wananchi wa kijiji hicho wakishiriki kubeba vifaa hivyo.Mkazi wa kijiji hicho, Beatrice Alphonce akiishukuru Serikali na MSD kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo.Mkazi wa kijiji hicho, Disifa Mdoe akipipongeza Serikali na MSD kwa kuwapelekea vifaa hivyo.Gari la MSD likiwa safarini kupeleka vifaa hivyo.

Wednesday 29 November 2023

TEWW yazindua programu ya IPOSA katika mikoa sita

Katibu Tawala Mkoa Singida, Dkt. Fatma Mganga, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Mfumo Rasmi (IPOSA) kupitia ufadhili wa Serikali ya Korea chini ya shirika la  Koica uliofanyika Novemba 28, 2023 mkoani  hapa. 

.....................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

TAASISI  ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imezindua  awamu ya pili ya Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya shule (MECHAV/IPOSA) kwa ufadhili wa Sh. Milioni 6 dola za Kimarekani zilizotolewa na  Serikali ya Korea Kusini  kupitia Shirika la Koica ambao umezinduliwa Novemba 18, 2023 mkoani Singida  ukilenga kuwakwamuwa vijana kielimu na kiuchumi.

Katibu Tawala Mkoa Singida, Dkt. Fatma Mganga akizindua mpango huo mkoani hapa kwa niaba ya mikoa sita ambayo mpango huo utatekelezwa kwa awamu ya pili  ametoa ushauri kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuangalia upya sera na sheria inayoelekeza mwanafunzi asiye hudhuria shuleni kwa muda wa siku 90 kufutwa baada ya kupoteza sifa za kuwa mwanafunzi.

Dkt. Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo  alisema  sheria hiyo imekuwa ikiongeza idadi kubwa ya vijana walio nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu  Changamani (IPOSA).

Alisema kuwepo kwa sheria hiyo kunaweza kuwafanya baadhi ya wazazi na walezi wasiopenda watoto wao kusoma kuwazuia wasiiende shuleni kwa muda huo kwa kuwa watakuwa wamejiondoa wenyewe hivyo kusababisha idadi kubwa ya watoto kuwepo mitaani bila ya kujua kusoma, kuandika na kuhesbabu.

Dkt. Mganga aliwataka maafisa elimu, watendaji wa Kata, maafisa Tarafa na viongozi wengine kufanya jitihada za makusudi katika maeneo yao ili kuwabaini watoto ambao hawaendi shuleni ili wajue kwanini wapo nyumbani na kuwarudisha shuleni.

Alisema Mkoa wa Singida wanafunzi wanaomaliza darasa la saba ufaulu wao haupo vizuri upo asilimia 76 jambo ambalo  si zuri ukilinganisha na mikoa mingine.

Alisema mpango huo wa IPOSA ni fursa kwa vijana walio nje ya shule kwa kuwa unalenga kupunguza idadi ya vijana walioko mitaani kwa kuwajengea stadi za maisha, stadi za ujasiriamali, stadi za Kusoma, Kuhesabu na Kuandika na stadi za Ufundi wa Awali na hatimaye kupata fursa za kujiajiri au kuajiriwa.

"Mpango huu umezingatia dhima ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya kutoa Elimu bora kwa wote, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, toleo la 2023 inayolenga pia kutoa mafunzo ya amali kwa vijana na Mpango wa Maendeleo ya Elimu," alisema Dkt.Mganga.

Alisema mpango huo unaendeleza utekelezaji wa azma ya Serikali kutoa Elimu kwa Watoto na Vijana kupitia mfumo rasmi na usio rasmi.

Aidha,  Dkt. Mganga alisema amefarijika kufahamu kuwa baada ya utekelezaji wa wa mpango huo katika mikoa 10  sasa wanaelekea kwenye upanuzi wa huo kwenye mikoa sita zaidi na kufikia mikoa 16 ya Tanzania bara na kuitaja mikoa hiyo sita kuwa ni Pwani,Tanga, Manyara, Simiyu, Singida na Shinyanga kwa ufadhili wa KOICA.

Alisema mikoa hiyo ilipatikana kwa kuzingatia uwepo wa vijana wengi kati ya umri wa miaka 14 na zaidi waliopo nje ya shule, utayari wa mikoa katika utekelezaji wa mpango huo , uwepo wa walimu wa ufundi na uwepo wa miundombinu pamoja na PPTCs.

Alisema mpango huo ulioanza kutekelezwa kwa ufadhili wa KOICA zitajengwa karakana mpya 30 kwa ajili ya mafunzo, ununuzi wa  vifaavipya vya kufundishia ufundi na kufadhili mafunzo ya muda mfupi ya walimu 240 na mafunzo ya diploma ya elimu ya watu wazima na teknolojia kwa walimu 120.

Aliongeza kuwa vilevile vitajengwa vituo 3 vikubwa vya mafunzo ya walimu watakaosoma diploma ya elimu ya watu wazima na teknolojia katika mikoa ya Tanga, Manyara na Shinyanga.

Alisema kwa hatua hiyo inadhihirisha jitihada walizozionesha na kuwapa imani wafadhili na kuendelea na awamu ya pili, ambapo pamoja na mambo mengine walifanikiwa kudahili vijana 12,000 (Me 5,406, Ke 6,594) kwa programu ya muda mrefu na 30,183 kwa programu ya muda mfupi katika kipindi cha miaka mitatu kwa Mikoa kumi ya Kigoma, Tabora, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Dodoma na Dar es salaam kwa ufadhili ya UNICEF na Mkoa wa Shinyanga kwa ufadhili wa Care International na Mkoa wa Rukwa kwa ufadhili wa Plan Internatioanal na   kuwa kwa awamu hii ya pili wamelenga kudahili vijana 52,000 mpaka ifikapo mwaka 2026.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Oscar Msalila alisema Mpango wa IPOSA ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya wizara hiyo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Taasisi ya Elimu ya Watu wazima na wadau wa maendeleo UNICEF.

Alisema kupitia mpango wa IPOSA vijana wenye umri kuanzia miaka 14 wameweza kujengewa stadi za ujasiriamali na stadi za ufundi wa awali ili waweze kujikomboa kiuchumi na kuchangia uchumi wa Taifa.

Alisema katika utekelezaji wa mpango huo wa  IPOSA  chini ya UNICEF, Care International na Plan International vijana waliofuzu mafunzo yao wameweza kuunda vikundi vya kijasiriamali ambavyo vimewawezesha kufanya biashara na kujipatia kipato.

Msalila alivitambulisha vikundi vichache vya IPOSA kutoka Mbeya na Kigoma ambayo vimeweza kuanzisha bidhaa za taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja pamoja na bidhaa za samani mbalimbali.

Alisema ubunifu wa bidhaa hizo ni muhimu kwa Taifa la Tanzania hasa kwa watu wa kipato cha chini, madhalani wale ambao si rahisi kumudu gharama za kununua taulo za kike zilizozoeleka ambazo bei zake kwa kiasi fulani ni kubwa kidogo.

Alisema zaidi ya kiwanda hicho cha taulo za kike  mpango huo umeweza kuzalisha vijana wabobezi katika fani ya umeme na wameweza kutengeneza mifumo ya kibunifu ambayo ni suluhisho wa ulinzi nyumbani.

Mkurugenzi Mkazi kutoka Taasisi ya Koica, Manshik Shin, alisema Koica ni chombo muhimu kwa Serikali ya Korea ambacho kinafanya kazi katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye nchi 46 duniani ikiwepo Tanzania na kuwa hapa nchini ilianzishwa rasmi mwaka 1991.

Alisema Koica ilifungua ofisi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2002 na kuwa katika nchi za Afrika Tanzania ni nchi ya pili kunufaika na miradi inayofadhiliwa na shirika hilo ambapo mpaka sasa jumla ya Sh.Bililioni 22 zimekuwa zikitolewa kufadhili miradi mbalimbali kila mwaka.

Shin alisema Koica imekuwa ikiisadia Tanzania Bara na Visiwani kwenye eneo la Elimu, Afya, Maendeleo ya Vijijini, Eneo la Jinsia, TEHAMA na masuala mbalimbali ya mtambuka.

Alisema katika sekta ya elimu Koica imekuwa ikifadhili shughuli za programu za ufundi, sayansi, uhandisi na hesabu ili kukuza uwezo wa vijana na waweze kujiajiri.

Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Dkt.Elpidius Baganda alisema mpango huo kwa Mkoa wa Singida umefika wakati muafaka kwani kuna vijana wenye umri kati ya miaka 14 hadi 19 zaidi ya 15,000 wenye sifa za kujiunga kwenye mpango huo, kunavija ambao hawakubahatika kwenda shule 672 na walioacha shule 1064, wanafunzi waliomaliza darasa la saba lakini hawakupa fursa ya kuendelea na masomo ni 12, 013, waliomaliza kwa kupitia MEMKWA ni 1260 na walioacha shule kwa changamoto mbalimbali zikiwepo mimba ni 398.Katibu Tawala Mkoa Singida, Dkt. Fatma Mganga, ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye uzinduzi wa mpango huo.Mkurugenzi Mkazi kutoka Taasisi ya Koica, Manshik Shin, akizungumzia jinsi shirika hilo linavyofadhili miradi mbalimbali hapa nchini.Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima,   Profesa Michael Ng;umbi, akizungumza kwenye uzinduzi huo.Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Oscar Msalila akizungumza kuhusu mradi huo.Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Profesa Sotco Komba, akizungumzia taasisi hiyo jinsi inavyoshiriki katika mpango huo.Mkurugenzi Idara ta Elimu Mbadala na Watu Wazima Zanzibar, Mashavu Ahamad Faga, akizungumza kwenye uzinduzi huo.Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ernest Hinju akizungumza kwenye uzinduzi huo.Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma,  Felician Ferdnand (kushoto) akiwa na  Mratibu wa Kituo cha Ufundi (TRC) cha Mbalizi Mkoa wa Mbeya Mhandisi Lwitiko Mwakatumbula ambapo walipata fursa ya kuelezea mafanikio ya mpango huo wa IPOSA katika mikoa yao kwenye uzinduzi huo..

Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Dkt.Elpidius Baganda, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye uzinduzi huo. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wanufaika wa programu hiyo wapo kwenye uzinduzi huo.

Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Viongozi meza kuu wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Singida Kanali Rhinoceros Magemeson,(kushoto)_ na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidi wa Polisi (ACP) Stella Mutabihirwa wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa.

Wasanii wa Kikundi cha Mbaramwezi wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.
Afisa Habari Manispaa ya Petronella Msechu (kushoto) na  Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya SingidaUpendo Naftali,wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma, Felician Ferdnand , akizungumzia mafanikio ya mpango huo mkoani humo.
Mratibu wa Kituo cha Ufundi (TRC) cha Mbalizi Mkoa wa Mbeya Mhandisi Lwitiko Mwakatumbula akielzea jinsi mpango huo ulivyowainua kiuchumi vijana mkoani humo.
Taswira ya uzinduzi huo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida , Yagi Kiaratu, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Katibu Tawala Mkoa Singida, Dkt. Fatma Mganga, akimkabidhi cheti Mwakilishi wa  Shirika la UNICEF, Pantalee Kapichi kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo kwa kusaidia katika maeneo mbalimbali.
Afisa Miradi ya Elimu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Selanda Zahoro Jamadari  akionesha cheti cha kutambua mchango wa TEA katika sekta ya elimu hapa nchini. 
Viongozi wa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja na waratibu wa uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na wadau wa maendeleo.
Picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Singida.