Friday 20 January 2017

WAZIRI ASHANGAZWA NA SHUTUMA DHIDI YAKE

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekutana na wadau wa sekta filamu nchini na kuoneshwa kusikitishwa juu ya shutuma dhidi yake na serikali kuwa wamekamata bidhaa haramu za wasanii na kuzirudisha kwa wamiliki kupitia mlango wa nyuma.
Akiongea wakati alipotembelea moja ya ghala la Kampuni ya Udalali ya YONO Waziri Nape amewatoa hofu wasanii na kuwaeleza kuwa bidhaa hizo za muziki na video ziko mahali salama na zitateketezwa bila kificho muda si mrefu

Akiongelea kuhusu sakata hilo Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba amewaasa wasanii kuacha tabia ya kushutumu viongozi bila kuwa na ushahidi wa kutosha

Katika Ziara hiyo Waziri Nape aliongozana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo na Wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA),COSOTA,Tume ya Ushindani wa Kibiashara(FCC) na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)

No comments:

Post a Comment