Random Posts

Rais kikwete akutana na Askofu mkuu wa Canterbury mjini Dodoma

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro). 8E9U6409 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby muda mfupi baada ya kufanya naye  mazungumzo katika ukumbi wa St.Gaspar mjini Dodoma.Askofu huyo alishiriki katika ibada ya kutawazwa kwa askofu mkuu mpya wa Kanisa la Anglikana nchini Tanzania Dkt.Jacob Erasto Chimeledya.

Rais Kikwete katika Sherehe za Kuapishwa Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania akutana na Skofu wa Cantebur


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania aliyemaliza muda wake Dkt.Valentino Mokiwa(katikati) akimtambulisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby muda mfupi kabla ya kuanza kwa ibada ya kumtawaza askofu Mkuu Mpya wa Kanisa hilo hapa nchini Askofu Jacob Erasto Chimeledya iliyofanyika katika Kanisa kuu la Roho Mtakatifu Dodoma.
8E9U6203
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini aliyemaliza muda wake Dr.Valentino Mokiwa akimtawaza aksofu Mpya wa Kanisa hilo Askofu Dkt. Jacob Erasto Chimeledya wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisa Kuu la Roho Mtakatifu mjini Dodoma leo.  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Dkt.Jacob Erasto Chimeledya wakati wa ibada ya kumtawaza kuwa askofu Mkuu iliyofanyika katika kanisa Kuu la roho Mtakatifu,mjijni Dodoma Leo(picha na Freddy Maro)

Post a Comment

0 Comments