Random Posts

KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI TANAPA CHAHITIMU MAFUNZO RUAHA NATION PARK


1Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya Ruaha kandokando ya mto Ruaha wakipewa  mafunzo hayo na  wakufunzi Martin Mthembu  kutoka taasisi ya African Field Rager Training Services ya Afrika kusini na Genes Shayo ambaye pia ni Mhifadhi TANAPA, kikosi hicho maalum cha TANAPA kilikuwa na askari 20 wamehitimu mafunzo hayo askari  19 moja hakufanikiwa kumaliza mafunzo kwa sababu za kiafya, Kivutio kilikuwa kwa askari mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia ameweza kufanya mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu  kutoka Afrika Kusini na akampa sifa na pongezi nyingi kwa uwezo wake kama mwanamke. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUAHA NATION PARK 3Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akirejea meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo hayo 4 
Askari wahitimu wa kikosi hicho kushoto ni Frank Anthon Malema na Mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 8 
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo 10Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Frank Anthon Malema kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Elisamehe Elisafi Mdeme kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 12Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimpongeza John Kijazi  baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo  13Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.14 
Martin Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa maelezo kwa Allan Kijazi  Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA  wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha Nation Park. 15 
Askari maalum wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakionyesha moja ya kazi zao wakati wakitafuta majangili katika hifadhi hizo 16 
Mmoja wa Askari wa kikosi hicho akilenga shabaha  17 
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Martin Mthembu akielezea mafanikio ya kikosi hicho katika kulenga shabaha kwa mkurugenzi wa hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi wa pili kutoka kushoto  wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Martin Loiboki na wa kwanza kushoto ni Dr. Christopher Timbuka Mhifadhi Mkuu Ruaha Nation Park 20 
Mkufunzi Martin Mthembu akielezea jinsi askari hao wanavyotakiwa kuwatafuta majangili huku wakiwa na maamuzi ya haraka bila kuchelewa na kutoua jangili ambaye hana madhara askari wa anatakiwa kufanya kazi yake kwa ufanisi lakini pia kulinda usalama wake yaani fanya kazi yako lakini rudi salama Askari mwanamke pekee Aikande Lema  akilenga shabaha huku mkufunzi huyo akiangaliaMkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi naye akimshuhudia askari huyo 23 
Askari Aikande Lema akirejea mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na mwalimu wake kwa mafanikio katika kulenga shabaha. 24 
Mto ruaha  25 
Mnyama tembo yuko hatarini kutoweka kutokana na majangili kuwauwa kwa wingi wakichukua

27  
pembe zake Twiga ni mojawapo ya wanyama ambao pia wanauliwa na majangili 28 
Mhifadhi wa Ruaha Nation Park Paul Banga akitoa maelekezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kabla ya kuingia mbugani jana kwa lengo la kujifunza utalii wa ndani na kujionea  wanyama mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi hiyo 29 
Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika geti la kuingilia kwenye mbuga ya Ruaha Nation Park

Post a Comment

0 Comments