Random Posts

KOCHA WA TIMU YA VIJANA ENGLAND KAZI KWISHA, FA YAGOMA KUMPA SHAVU LINGINE!!

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21,  Stuart Pearce kibarua chake kimefika ukingoni baada ya kuifundisha timu hiyo kwa miaka sita.
Pearce ameambiwa na chama cha soka cha England, FA kuwa hatapewa ofa ya mkataba mpya baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika siku 12 zijazo.
Tayari kocha huyo ameshawaambiwa wasaidizi wake kuwa anajiandaa kuachana na majukumu hayo ya kukinoa kikosi hicho.
Nafasi ya Pearce imekuwa hatihati baada ya kufanya vibaya katika michauno ya vijana kwa mataifa ya Ulaya mwaka huu.
Katika michuano ya EURO 2013 inayofanyika nchini Israel, England ilipoteza michezo mitatu dhidi ya Italy, Norway na wenyeji Israel.
Ingawa Pearce alionesha nia ya kuendelea na majukumu yake baada ya kupoteza mchezo wa kwanza mjini Tel Aviv, lakini baada ya mkutano na waandishi wa habari kumalizika, chama cha soka nchini England FA kilisema haitawezekana.
Final act: Pearce oversaw England Under 21s' woeful European Championship campaign 
Kazi kwishwa: Pearce akikiongoza kikosi chake kwa mara ya mwisho katika fainali za vijana kwa mataifa ya Ulaya
Limp exit: Pearce's Young Lions lost all three game in Israel 
Kipondo tu: Pearce na kikosi chake cha Simba wadogo wamepoteza michezo mitatu
Moving on: Outgoing FA chairman David Bernstein chats to Pearce in Israel  
Mwenyekiti wa FA , David Bernstein akiongea na Pearce nchini Israel
 FA wanajiandaa kutafuta kocha mpya huku Gareth Southgate na Michael Appleton wakitajwa zaidi kurithi mikoba ya Pearce.
Pearce alianza kazi mnamo mwaka 2007 na ameingoza England kushinda vikombe vinne mfululizo, hivyo kusifiwa na mwenyekiti wa FA kuwa kocha huyo anastahili heshima kwa kazi yake nzuri, lakini kwa sasa imefika mwisho.

Post a Comment

0 Comments