
Wasanii kutoka Nigeria, Panshak
Zamani, anayejulikana zaidi kwa jina la Ice Prince(Pichani kulia, pamoja
na David Adedeji Adeleke(Pichani chini kabisa), wanatarajia kuwa
wasanii wakubwa watakaoitikisa Kenya mwishoni mwa wiki hii katika
tamasha kubwa la muziki na mitindo linalojulikana kwa jina la Boombataa
Festival.Wasanii pekee kutoka kernya watakaoshiriki tamasha hilo ambalo
ni la kwanza kufanyika, ni Victoria Kimani, Sound Afrique Band na Sauti
Sol, huku wasanii wengine wakubwa watakaoonekana katika tamasha hilo
wakitajwa kuwa ni Monster Djs na Purpl Dj.
Kampuni ya Adrenaline, ambao
ni waandaaji wa tamasha hilo wameiambia mwananchi kwamba litakuwa
tamasha la mfano kwa Afrika Mashariki nzima na linatarajia kuvuta maelfu
ya watu kuhudhuria kutokana na kuleta wasanii wakubwa na wa kimataifa.
Ice Prince anayetamba na
nyimbo kama Oleku, Olofofo, Superstar na Baby anatarajia kufanya onesho
lake la kwanza nchini Kenya tarehe 27 ya mwezi huu ambapo ataambatana na
mwanamuziki mwenzake Davido ambaye pia anajulikana kupitia wimbo wake
mpya wa Gobe, uliovunja rekodi ya kuangaliwa mara milioni moja kwa
dakika 25, ulipowekwa kwenye mtandao wa Youtube.
Homa ya kuwasili kwa wasanii
hao imesababisha wasanii kutoka kenya kupania tamasha hilo huku dhamira
ikiwa kuwafunika wanigeria hao wanaotamba katika medani ya muziki
duniani kote ambapo SautiSol, wamekuwa waki’twee’ mara kwa mara
kuongelea jinsi watakavyoonesha maajabu katika tamasha hilo.
Tamasha hilo kubwa na la kimataifa linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ngong Race Course
0 Comments