Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Ikiwa
ni mikakati wa kujiandaa na msimu mpwa wa ligi kuu soka Tanzania bara
unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu, klabu za Azam fc
na Ashanti United zinatarajia kushuka dimbani kuoneshana kazi hapo kesho
uwanja wa Chamazi Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Afisa
habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga amethibitisha kuwepo kwa mechi
hiyo na kudai kuwa itakuwa nafasi nzuri kwa benchi la ufundi kutazama
uwezo wa wasukuma kabumbu wao baada ya mazoezi ya siku nyingi.
“Tutakabiliana
na Ashanti hapa nyumbani, ni mchezo wa kirafiki wa kawaida, lakini ni
muhimu kwa makocha wetu kupima uwezo wa kikosi chao, hivyo mashabiki
waje waone mchezo huo”. Alisema Jafar.
Jafar
aliongeza kuwa mazoezi yao yanaendelea vizuri, huku kocha mkuu Sterwart
John Hall akiwa na mpango mzito wa kutwaa ubingwa msimu ujao.
“Malengo
yetu ni kuhakikisha tunatwaa taji la ligi kuu msimu ujao, lakini
ukumbuke kuwa kwa mara nyingine sisi ni wawakilishi wa Tanzania katika
michunao ya kombe la shirikisho barani Afrika mwakani, hivyo maandalizi
yetu yamelenga ligi kuu na michauno ya kimataifa”. Alisema Jafar.
Afisa
habari huyo wa wana lambalamba alisisitiza kuwa toka awali
walishatangaza kuwa Azam fc imekuja kuleta mapinduzi ya soka la
Tanzania, na nia yao iko pale pale.
“Sisi
tunafanya jitihada kubwa ya kuandaa kikosi bora cha mapinduzi ya soka
la Tanzania na kuua ufalme wa Simba na Yanga, hakika kila kitu
kitawezekana kutokana na mipango mizuri ya benchi la ufundi pamoja na
viongozi wa klabu, cha msingi Watanzania watupe sapoti kubwa zaidi”.
Alisema Jajar.
0 Comments