Mwenyekiti
wa chama cha wanasheria wanawake Tanzania TAWLA Bi. Aisha Zumo Bade (wa
tatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na Wanasheria wenzake wakiwa tayari
kuwapatia futari watoto yatima wapatao 80 wanaolelewa katika
Kituo cha MWANA OPHANS CENTRE ,Kilichopo vingunguti Manispaa ya Ilala
jijini Dar es salaam, ambapo zoezi hilo lilienda sambamba na kukabidhi
msaada wa vifaa venye thamani ya Shilingi Milion 2,600,000
Mwenyekiti
wa TAWLA Aisha Zumo Bade akimpatia futari mmoja wa wafanyakazi wa TAWLA
kwa ajili yakuwapatia watoto wa kituo cha MWANA OPHANS CENTRE.
Watoto wakifuturu futari ilioandaliwa na chama cha wanasheria wanawake Tanzania TAWLA.
Mwanasheria, Nasieku Kissambu akipata futari pamoja na watoto wanaolelewa na kituo hicho
Mwenyekiti wa TAWLA, Aisha Zumo Bade akimlisha futari mmoja wa watoto wa kituo cha MWANA OPHANS CENTRE .
Wafanyakazi
wa TAWLA wakishusha baadhi ya vyakula na vifaa mbalimbali kwenye kituo
cha kulelea watoto yatima cha (MWANA OPHANS CENTRE). Waliosimama wa
kwanza kutoka kulia ni Bi,Nasieku Kissambu na wapili kutoka kulia
anayeandika ni Bi Tike Mwambipile, wote ni viongozi kutoka TAWLA

Mwenyekiti
wa TAWLA, Bi Aisha Zumo Bade (katikati) mjumbe wa Halmashari kuu TAWLA,
Bernadetha Mkandya (wakwanza kushoto) wakimkabidhi moja ya vifaa Mlezi
wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha MWANA OPHANS CENTRE, Bi,Sada
Omariy
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMONI WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM)
0 Comments