Random Posts

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN LEO ALIKUWA WILAYA YA ITILIMA MKOA MPYA WA SIMIYU

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa kahawa mara baada ya kukaribishwa na wananchi katika kijiji cha Budalabuhega wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha chama na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi katika wilaya ya Itilima mkoa mpya wa Simiyu leo ambapo amekagua miradi mbalimbali na kuzngumza na wenyeviti wa matawi na mashina katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kufungua mashina, kesho ataendelea na ziara yake katika jimbo la Bariadi mjini. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-ITILIMA SIMIYU 2 
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Budala Budalabuhega leo. 5 
Huu ndiyo uhalisia wa maisha Mtoto huyu ambaye hakufahamika jina lake akiwa amembeba mdogo wake huku akiwa amemshika mkono mwingine katika moja ya vijiji tulivyopitia katika ziara ya leo wilayani Itilima. 6 
Hili ni jengo la zahanati ya kijiji cha Nangale kata ya Ndololezi Kinana alikaguikagua pia 10 
Wana CCM wa kata ya Migato wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza nao katika shina namba 15 shuleni kata ya Migato. 16 
Ndugu Nape Nnauye akipanda mti katika eneo la halmashauri ya Itilima  30 
Mkutano wa ndani ukiendelea chini ya mti. 31 
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo. 33 

Post a Comment

0 Comments