Random Posts

MWENYEKITI VIJANA CCM AONYA UTEUZI WA WAGOMBEA



Na Bernard James
Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis amesema kila Mwanachama ana wajibu wakumsimamia mgombea anaeteuliwa na chama katika uchaguzi wa nafasi mbalimbali ikiwamo uraisi.
Amesma kutokana na hali ni vyema kila mwana CCM ahakikishe natekeleza suala hilo kwa umakini kwa kuchagua mtu ambye atakuwa na manufaa kwa chama na wananchi kwenye majimbo yao.
Kauli hiyo alitoa Dar es salaam juzi katika ziara yake ya siku mbili katika Wilaya ya Kinondoni.
Alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa kila mwanachama anatakiwa kuwapima wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kama wana sifa za kutosha kabla ya kufanya uwamuzi kwa vile kufanya hivyo kutakifanya chama hicho kushinda uchaguzi wa mwaka 2015.
“Mgombea atakayechaguliwa na wana CCM ndiyo atakuwa huyo huyo nasi tutapambana kuhakikisha  anashinda uchaguzi kwa kumnadi kwa wananchi.
“Ni kwa hapa mna fursa ya kujiandaa sasa na si vinginevyo na kila kijana ahakikishe kuwa jimbo hili linarejea katika mikono ya CCM kwa sababu sie ndiye tuliosababisha mbunge wa sasa kushinda kutokana na hali ya makundi ndani ya chama chetu,alisema Khamis.







 Msanii Babu naye akitoa burudani
 Wanachama wa CCM wakijimwaga uwanjani







Post a Comment

0 Comments