Na Bernard James
SERIKALI
imetakiwa kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wazawa kwenye sekta ya mafuta na gesi
kwa kuwa walio wengi wanauwezo,mitaji na elimu hiyo jambo litakalosaidia kuinua
uchumi wan chi na wa mwananchi mmoja mmoja.
Pia,wawekezaji
hao wazawa,wamelaani kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na
Madini,Prof.Sospiter Muhongo iliyoonekana imewadhalilisha wazawa kwa kuwaambia
kuwa hawana mitaji ya kuwekeza kwenye sekta hiyo inayokuwa kwa kasi hivi sasa
nchini.
Akizungumza
kwenye mkutano wa pili wa wadau wa mafuta na gesi uliomalizika jana jijini Dar
es salaam na kushirikisha wadau kutoka mataifa mbalimbali,Mkurugenzi wa kampuni
ya huduma za mafuta na gesi ya JAR,Erick Mashauri,alisema hivi sasa wazawa
wamejipanga ili kuhakikisha sekta hiyo inawanufaisha waTanzania badala ya kuwa
laana.
Mashauri
aliishauri serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya uwekezaji ili kuepuka
madhara makubwa kama yakiyotokea kwenye sekta ya madini ambapo wananchi walio
wengi hawanufaiki na uwekezaji huo hivyo kuzidisha migogoro baina ya pande hizo
mbili.
Mwekezaji
huyo ambaye pia anajishughulisha na sekta ya utalii kwa kukodisha magari na
kukambika,inamilikiwa kwa asilimia mia moja na wazawa huku ikiwa imeajiri
wafanyakazi zaidi ya 70 hivyo kuwa ni moja ya kampuni zenye kuleta tija kwa
kuhakikisha uchumi wan chi unakuwa.
“Utafiti na
uchimbaji mafuta na gesi unaweza kufanyika na kuisha lakini inapaswa
tujiulize,wananchi wamefaidika vipi na uwekezaji huo?Naomba tuhakikishe
uwekezaji huo unakuza pato la mtanzania kwa kuwa Tanzania siyo masikini kama
tunavyodhani”,alisema Mashauri.
Aliongeza
kuwa,”kama tukiendeleza dhana ya kuwaona wawekezaji toka nchi za nje kuwa ndiyo
wenye uwezo na mitaji ya kuwekeza,tutashangaa nchi zao zinazidi kutajirika huku
sisi tukilazimika kwenda kuomba misaada ambayo mara nyingi huja na masharti
mengi na magumu lakini wakati umefika sasa kuwaamini wazawa kuwa nao wanaweza”.
Aidha,kampuni
hiyo tayari imekwisha wekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 300 kwenye sekta
hiyo hivyo hakuna haja ya kuwaona watanzania kama masikini wasiokuwa na mitaji
mikubwa.
Alitolea
mifano ya baadhi ya huduma ambazo serikali inatakiwa kuwapatia wazawa
wazitekeleze kuwa ni pamoja na huduma za usafi,upishi,ufundi na za mahusiano
ambazo zote wanaweza kuzifanya wazawa.
“Utashangaa
mafundi magari wanatoka nje ya nchi,wafanya usafi na hata wapishi,jamani hivi
kweli sisi hatuwezi kupika au kurekebisha magari?Naiomba serikali hii
ihakikishe inaorodhesha shughuli zote
ambazo zitafanywa na wageni na zile za wazawa ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya
maana”.
Wakati ombi
hilo likitolewa na Mkurugenzi huyo,hali halisi inaonesha kuwa nwazawa wengi
hawaaminiki kupewa miradi mikubwa ya uwekezaji kwani wakati wa michakato ya
kuuzwa kwa baadhi ya mashirika ya umma wengi wao waliomba lakini hawakupata
hivyo kuwavunja moyo wa biashara ya ushindani ikiwa ni pamoja na kutoaminika
kwenye uwekezaji wa kimataifa.
mwisho
0 Comments