Mratibu wa matembezi Bw.Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma akiwa katika muonekano wa picha.
NCHI YANGU; WAJIBU WANGU 11.01.2014 (takribani 200km)Dar es
Salaam mpaka Morogoro.
Ndugu zangu Watanzania, naomba kuwasalimu, katika jina la
Mlima mrefu ukaitwa Kilimanjaro, visiwa vya marashi ya karafuu Zanzibar,
Serengeti, Ngorongoro, mapango ya Amboni, pwani zilizojaa kubwa shani na ardhi
yenye wingi wake gesi na madini, kwa hakika umaskini/ufukara wetu upo katika
fikra zetu.
Kuanzia tarehe 11.01.2014 Matembezi ya hiyari kwa miguu kutoka
Dar es Salaam mpaka Morogoro yataanza rasmi yakikadiriwa kuchukua siku
zisizozidi kumi, lengo kuu likiwa ni kuhamasisha, kukumbushana na kuenzi Umoja,
Amani na Utulivu kama Taifa moja likaitwa Tanzania ilhali juhudi yakinifu
kuanzia ngazi ya mwananchi mmoja mmoja, familia, kaya, wilaya mpaka Taifa
kujivika jukumu la kufahamu, kupambanua, kudadavua na mwisho wa siku
kushirikiana kupitia njia za makusudi kuhakikisha maliasili na utajiri wa Taifa
hili jadidu unamnufaisha kila Mtanzania, huku masuala ya Elimu, Afya, Ustawi wa
Jamii, Ujasiriamali na Taaluma yakitiliwa mkazo pasi kuachwa kando.
Matembezi haya yanatarajiwa kuwa na vituo kadhaa vikiwemo ;
Kibaha, Mlandizi, Vigwaza, Chalinze, Mikese na kumalizia Morogoro, tunatarajia
ndugu zetu Watanzania tujikimu kwa mahitaji kadha wa kadha tuwapo safarini,
Nchi ikiwa Yetu, Wajibu ukiwa Wetu na UTAIFA tukiuweka na kuutanguliza mbele.
Mpaka sasa matembezi haya ya hiyari yenye kauli mbiu Nchi Yangu, Wajibu Wangu : UTAIFA KWANZA hayajapata
mdhamini yeyote na maandalizi yote mpaka sasa ni kufikia lengo la matembezi
kama Tanzania iliyo moja bila kujali itikadi, imani, dini, asili ama hata
tofauti za kiuchumi miongoni mwetu na kuangaza katika Tanzania yenye kutoa
nafasi kwa kila Mtanzania.
Kwa hakika maandalizi ya msingi yamekamilika na tarehe
11.01.2014 ndoto yetu ya kufanya matembezi ya hiyari yatafikisha ujumbe ulio wa
Amani na Ustawi wa Taifa letu itachukua nafasi na kuwa halisia.
Nchi Yangu, Wajibu
Wangu : UTAIFA KWANZA
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma
+255-772-54- +255-62/784-311056,
Barua Pepe: kwetutanzania@yahoo.com,
Ukurasa: www.facebook.com/kwetutanzania.
0 Comments