Na Datus Boniface, Jeshi la Polisi Iringa
JESHI
la Polisi mkoa wa Iringa limepiga marufuku kwa Mwananchi kuhudhuria mikutano ya
kampeni wakiwa na marungu na mapanga hasa wakati huu wa kampeni za kuwania kiti
cha Ubunge Jimbo la Kalenga.
Aidha,
limewataka kuacha mara moja wataka wamiliki wa Malori kubeba wafuasi na wapenzi
wa vyama vya siasa kwa lengo la kuwapeleka katika mikutano ya kampeni.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Kakamba alisema Jeshi la Polisi halitavumilia
mtu atakayevunja sheria katika kipindi hiki cha Kampeni na uchaguzi.
"Uzoefu
tuliopata katika chaguzi ndogo za Udiwani wa Kata za Nduli, Ibumu na Ukumbi
ziligubikwa na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ikiwemo wafuasi wa
vyama mbalimbali kushambuliana pamoja na kutembea na marungu na
mapanga"alisema
Aliongeza
kwamba, katika chaguzi hizo yalitokea matukio mbalimbali yakiwemo ya
kuingiliana ratiba za kampeni na viwanja na pia kujichukulia sheria mkononi kwa
kuwapiga watu bila sababu za msingi au kwa hisia kwamba ni wapinzani wa vyama
vyao.
Kaimu
Kamanda alisema, tayari kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Kalenga zimeshaanza
tangu Februali 19 na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimezindua
kampeni zake Februali 22 kwa Kata ya Kalenga.
Alisema
Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kampeni hizo zinafanyika kwa
amani na utulivu ambapo pia Polisi watasimamia vizuri ulinzi siku ya uchaguzi
hadi kutangazwa kwa matokeo.
Hivyo,
aliwataka viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo
pamoja na wafuasi wao kufanya kampeni za kistaarabu bila fujo.
Alifafanua
kuwa, kila chama kizingatie ratiba na muda wa vibali wa kumaliza mikutano
ya kampeni.
Alitumia
fursa hiyo pia kuwaomba wadau wa Ulinzi na Usalama kutoa ushirikiano kama
walivyofanya katika chaguzi zilizopita, kwa lengo la kudhibiti vitendo vyenye
kupelekea kuvuruga kampenzi na uchaguzi kwa ujumla.

0 Comments