Mamia
ya akina mama na wananchi wa Jiji la Mwanza wakishiriki katika sherehe
ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa
Nyamagana ambapo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi
katika shughuli hiyo tarehe 8.3.2014.
Ngoma
ya asili ya kabila la Wasukuma ya Bugobogobo ikichezwa kwa umahiri
mkubwa hata kumfanya Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni
rasmi katika sherehe hiyo kushuka jukwaani na kuicheza na baadaye
kumzawadia mtoto wa kikundi hicho kutoka Mji wa Magu wakati wa sherehe
za uzinduzi wa upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika
katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza tarehe 8.3.2014.

Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akizindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi
wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani katika sherehe
iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza tarehe 8.5.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Nestory
Masalu kutoka hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye alikuwa akiwapima
akina mama katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko katika wilaya ya
Ilemela mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani
ya mlango wa kizazi katika uwanja wa Nyamagana na kutembelea kituo
hicho ambapo wanawake wengi walijitokeza kwa ajili ya kupima.
Mke
wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya
wanawake na wananchi waliokusanyika katika kituo cha Afya cha Buzuruga
kilichoko wilayani Ilemela, Mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi
upimaji wa saratani ya kizazi kwa akina mama tarehe 8.3.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI
0 Comments