Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Enjinia Bashir Mrindoko akitoa hotuba kwa niaba ya
Profesa Jumanne Magembe wa Wizara hiyo wakati akizindua mradi wa maji safi na
salama Afya na Mazingira Uzinduzi huo uliofanyika katika shule ya Msingi
Mbagala Kuu Machi 12,2014 jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Ubelgiji Nchini Tanzania, Koenraad Adam akielizea mradi huo utakavyo
wanufaisha wakazi hao.
Wageni
walikwa mbalimbali wakishuhudia Uzinduzi wa maji safi na salama Afya na
Mazingra.
Wafuzi
wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu wakiwa tayari kushuhudia Uzinduzi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Enjinia Bashir Mrindoko (katikati), akikata utepe
kuzindua rasmi Uzinduzi wa maji safi na salama Afya na Mazingra (wakwanza
kushoto), Balozi wa Ubelgiji Nchini Tanzania Koenraad Adam, na anaefuatia
mwenye shati la bluu Mwakilishi wa Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU), Eric Beaume
(wakwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Maendeleo Ubelgiji, Peter Moors.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Enjinia Bashir Mrindoko akimtuisha ndoo ya maji mkazi
wa eneo hilo mara baada ya kuzindua.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu wakiwa na mabango yenye ujumbe wa maji na mazingra wakipita
mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma Makonde Dansi kikitoa
burudani wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa maji safi na salama Afya na
Mazingra.
HABARI PICHA
NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR
ES SALAAM
............................................................................................................................................................
WANANCHI wa Mbagala Kuu wameilalamikia Shirika la Umeme Tanzania
Tanesco kutokana na uzalishaji mdogo wa umeme unaosababisha visima vya maji
kushindwa kuzalisha maji ya kutosha.
Akisoma risala ya wananchi Lydia Changula alisema tatizo la maji
safi na salama limeweza kutatuliwa kwa asilimia 100,kikwazo kikubwa ni umeme
mdogo unaosababisha kuzalisha maji chini kiwango.
Alisema mradi wa maji safi na salama,Afya na
Mazingira umesaidia kuwepo kwa tenki za maji 16 ambazo zimesambazwa
katika vituo 381 vinavyotoa huduma ya maji safi na salama kwa watu
laki moja na sabiini elfu.
“ Mradi huu umesaidia ujenzi wa vyoo 21 kwa
shule za msingi vyenye matundu 138 na kufanikiwa kukarabati matundu 8 hali
iliyosaidia kupatikania kwa huduma bora za vyoo”alisema Changula.
Akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Maji Profesa.Jumanne
Maghembe katibu Mkuu wa wizara hiyo Enjinia
Bashir Mrindoko alisema mradi huo umetumia zaidi ya bilioni 15
ambazo zimetumika kwa miradi 15 katika manispaa tatu.
Alisema fedha hizo zilitolewa kwa ushirikiano wa nchi ya
Tanzania,umoja wa Europe pamoja na ubelgiji ambapo lengo kubwa la kutekeleza
mradi huo ni kuweza kupunguza kero ya maji nchi hususani kwa mama na mtoto.
“Malengo ya serikali ni kuhakikisha kero ya maji nchini
inapungua kama sio kumaliza kabisa hadi kufikia mwaka 2015 na kuhakikisha
wananchi wote wanapata maji safi na salama”,alisema Mrindoko.
Alisema mradi huo wa maji utasaidia wananchi wanaokaa pembezoni
mwa Dar es saalam kwa asilimia 55 na kusisitiza kuwa mradi huo ni zaidi ya matumizi
ya wizara lazima itunzwe.
Alisema serikali haitarajii kuona wananchi wanawaachia wajanja
kujiunganishia maji hayo kiholela huku matatizo ya maji yakiongozeka badala
yake watumie sheria zinazofaa ili kuweza kuunganishiwa maji.
Akisoma hutuba kwa wananchi Balozi wa Ubelgiji Koenraad Adam
alisema mradi huo wa maji ni sehemu kuu kwa nchi ya Tanzania na Ubelgiji.
Alisema bila ya maji safi na salama katika taifa hakuna maisha
na kuwataka wananchi wasidanganywe na wajanja wachache watakaotumia maji vibaya.
“Mimi ni raia wa ubelgiji licha ya kwamba nchi yangu ni ndogo
sana lakini miongoni mwa vitu tulivyobarikiwa ni maji na ndio maana na sisitiza
matumizi ya maji yatumike kwa uangalifu,musisubiri kila kitu kufanyiwa na
serikali lazima na nyinyi nwenye mubadilike”,alisema Adam.








0 Comments