TANZIA!
Mwanamuziki Mkongwe nchini Tanzania, Muhidin Gurumo amefariki dunia leo
hii majira ya saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kwa muda mrefu Mzee Gurumo amekuwa akisumbuliwa na maradhi mpaka siku ya leo alipotangulia mbele ya haki.
Hili
ni pengo kubwa katika muziki wa dansi nchini kwani kwa muda wote wa
uhai wake amekuwa akitoa mchango mkubwa katika kuuendeleza muziki huo.
Kifo
cha Gurumo kimewagusa wadau mbalimbali wanaopenda na wasiopenda muziki
kutokana na umaarufu wake mkubwa aliojingea kupitia kipaji chake
kikubwa.
Mtandao huu utaendelea kukupatia taarifa zaidi kadri muda unavyozidi kwenda.
Tafadhali endelea kufuatilia kwasababu timu nzima ipo njiani kueleka nyumbani kwa marehemu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Gurumo mahala pema peponi. Ameni.