Random Posts

KAMPUNI YA SMILE COMMUNICATIONS TANZANIA YAENDESHA DROO YA MWISHO NA KUPATA WASHINDI

001Mkuu wa Mauzo wa  Kampuni ya Smile  Communications Tanzania, Linda Chiza akiongea na waandishi wa habari Aprili 1, 2014 makao makuu ya Smile Communication yaliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.002Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika hafla ya kuwatangaza washindi wa “Shinda iPad” ambapo wateja 13 washindi wa droo hiyo wamejinyakulia iPad kila mmoja.003Mkuu wa Mauzo na Usambazaji na Masoko Kampuni ya Smile  Communications Tanzania Bw. Lawrence Ndimbo akichanganya karatasi kwenye boksi maalumu ili kumtafuta mshindi wa droo hiyo, wanaoshuhudia (katikati), Mkuu wa Mauzo wa  Kampuni ya Smile  Communications Tanzania, Linda Chiza, na Muffadal Essaji wa Kampuni hiyo.004(2)Mkuu wa Mauzo na Usambazaji na Masoko Kampuni ya Smile  Communications Tanzania Bw. Lawrence Ndimbo (katikati), Mkaguzi Mwandamizi wa Michezo ya Kubahatisha (TGB), Abdala Hemedy, na kushoto Msaidizi wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw.Muffadal Essaji.005Mkuu wa Mauzo na Usambazaji na Masoko Kampuni ya Smile  Communications Tanzania Bw. Lawrence Ndimbo (kulia), akimpigia simu mshindi wa droo hiyo ili kumfahamisha kama ameshinda (katikati), Mkaguzi Mwandamizi ya Michezo ya Kubahatisha (TGB), Abdala Hemedy, na kushoto Mkuu wa Mauzo wa  Kampuni ya Smile  Communications Tanzania, Linda Chiza.
HABARI PICHA-NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Kampuni ya Smile communications Tanzania  (Smile), inayotoa huduma ya  intaneti Dar es Salaam na Arusha, leo imeendesha droo ya mwisho katika droo za wiki kuhitimisha promosheni ya “Shinda iPad” ambapo wateja 13 washindi wa droo hiyo wamejinyakulia iPad kila mmoja.
Katika ofa hiyo, wateja wapya wa Smile walitakiwa kununua kifaa cha Mi-Fi au Router kutoka katika maduka au vibanda vya Smile ndani ya mwezi Machi   ili kupata nafasi ya kushindania moja kati ya iPad 13 zilizokuwa zikishindaniwa.
Promosheni hiyo iliyokuwa ikisimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (TGB) imewazawadia wateja tisa (9) kutoka Dar es salaam na (4) kutoka Arusha. 
Droo ya mwisho imefanyika leo makao makuu ya Smile Dar es Salaam ambapo washindi wanne wa mwisho wamechaguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Linda Chiza, amesema kampuni yake imetoa zawadi ya toleo jipya la iPad lililowezeshwa katika teknolojia ya 4GLTE zikiwa na vivurushi vya  GB5 za intaneti.
“ Tunawapongeza washindi na wote walioshiriki na kutembelea kwenye sehemu tunazotolea huduma” alise Chiza na kuongeza kuwa “ kila mwezi tunakuwa na kitu cha kuwafanya watabasamu. Tutawajulisha nini kinafuata”.