Random Posts

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KITUO CHA WALEMAVU CHA RASIBURA NA KUTOA ZAWADI YA PASAKA


IMG_8620 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwenye kituo cha walemavu cha Rasibura na Ndugu Simon Mnimbo, Mkurugenzi wa Shirika la Caritas la Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi wakati Mama Salma alipokitembelea kituo hicho tarehe 20.4.2014, siku ya Pasaka kwa ajili ya kuwapelekea zawadi  za sikukuu.
IMG_8624  
Jengo linalotumika kwa makazi ya walemavu huko Rasibura, katika Mji wa Lindi likiwa katika hali mbaya ya uchakavu. Jengo hilo awali lilikuwa likitumiwa kama gereza na Jeshi la Magereza la Lindi na baadaye kukabidhiwa kwa Idara ya Ustawi wa Jamii na ndipo walipoamua kutumia kama jengo la kuwatunzia watu wenye ulemavu.IMG_8627 IMG_8628 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali za jengo la kuwatunzia walemavu huko Rasibura Mjini Lindi akiongozwa na Mlezi wa Kituo hicho Ndugu Simon Mnimbo kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi tarehe 20.4.2014.
IMG_8679 
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiongea na watu wenye ulemavu mbalimbali wanaoishi Rasibura baada ya kutembelea sehemu mbalimali za jengo lao. Mama Salma aliwatembelea walemavu hao wakati wa sikukuu ya pasaka na kuwapa zawadi mbalimbali za sikukuu hiyo tarehe 20.4.2014.
IMG_8693  
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na mtoto Idd Mohamed Chitawala ambaye ni mlemavu wa macho anayeishi katika kituo cha rasibura pamoja na Baba yake Mzazi Bwana Mohamed Chitawala.IMG_8701 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi Kiongozi wa Kituo cha walemavu cha Raisbura Bwana Mohamed Chitawala baadhi ya vyakula alivyowaletea- mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukai, soda na vinginevyo wakati alipotembelea kituo cha walemavu cha Rasibura huko Lindi siku ya Pasaka tarehe 20.4.2014.
Picha na John Lukuwi