Random Posts

MWANAMUZIKI MAARUFU WA SKYLIGHT BAND MAREHEMU CHILL CHALLA AZIKWA JANA JIJINI DAR

 Waombolezaji wakiwa msibani Jana kushoto mwenye tisheti nyeusi ni Mratibu wa Skylight Band
William Malecela akijadili jambo na Mkurugenzi wa Skylight band ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.
Baadhi ya waombolezaji wakibadilishana mawazo Katikati ni Mwanamuziki wa Skylight band Joniko Flower
Waombolezaji wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubili mwili wa marehemu Kufika,Mwenye Baibui nyeusi ni mke wa Chicago Matelephone na wanamuziki wa Skylight band
Mkurugenzi wa Skylight Band akijadili jambo na Aneth Kushaba ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.
 
Gari iliyobeba Mwili wa marehemu Chill Challa likiwasili Nyumbani kwa marehemu
 
Ndugu na Jamaa wakishusha Mwili wa marehemu Chili Challa
 
Mwili wa Marehemu ukishushwa kwa ajili ya ibada
Mchungaji wa kanisa alipokuwa Anasali marehemu akiongoza ibada ya kumuombea Marehemu Ayoub Songoro maaru Chill challa aliyekuwa mwanamuziki na mpiga Gita wa Skylight Band.
Misa ya kumuombea Marehemu akiendelea Nyumbani kwake Mwananyamala
 
Mke wa marehemu akiwa na majonzi
Meneja wa bendi Ya Skylight Aneth Kushaba akiaga mwili wa marehemu
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
 
Ndugu wa Marehemu wakiweka Shada la maua
 
Mpiga Gita mahiri wa bendi ya Skylight Chill challa amezikwa jana kwenye makaburi ya Mwananyamala kwa kopa na mamia ya watu na wanamuziki wenzie.Marehemu Chill challa alifariki Tar 17-04-2014 hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Chanzo cha kifo cha marehemu ni shinikizo la damu ambapo kabla ya kifo chake alikuwa katika afya njema,lakini Usiku wa Tar 16 marehemu alidondoka gafla bafuni na ndipo alipkimbizwa hospitalini.
Madaktari walijitaidi kwa kila hali na mali kuokoa uhai wa marehemu lakini ilishindikana kutokana na shinikzo la damu kuwa kubwa sana na ndipo Chill challa akafariki dunia,Marehemu Chill challa ameacha Mke na watoto wawili,Marehemu alikuwa ni mpiga gita mzoefu na mahiri ambaye amepitia karibu bendi zote kubwa na kongwe nchini kama Akudo,Fm academia Nk.
uongozi mzima wa Skylight band unawashukuru wale wote waliojitoa kwenye msiba huu na Mungu awabariki.
PICHA ZOTE NA DJ SEK BLOG