Rais Jakaya Kikwete akikata utepe huku Balozi wa Uholanzi hapa
nchini Mhe Jaap Frederiks na Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe
wakiwa wameshikilia utepe huo wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa
upanuzi wa Uwanja mkubwa wa ndege wa J.K.Nyerere Terminal 3 utakaoweza
kuhudumia abiria milioni 7.500.000 kwa mwaka, Ujenzi huo umefadhiliwa na
serikali ya Uholanzi na unatarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka huu,
kutoka kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Miundo mbinu
Peter Serukamba, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Juma Kapuya na
Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Injinia Suleiman Suleiman na
kutoka kushoto ni Didas Masaburi Meya wa jiji la Dar es salaam, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik na Naibu waziri wa Uchukuzi Mh. Dr.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Uholanzi hapa
nchini Mhe Jaap Frederiks wakifunua pazia huku Waziri wa Uchukuzi Dr.
Harrison Mwakyembe katikati na viongozi wengine wakipiga makofi wakati
wa uzinduzi wa ujenzi wa uwanja huo.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali huku akiwa ameongozana na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya
viongozi baada ya kuwasili katika uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi wa
Mamlaka ya viwanja vya ndege Injini Suleiman Suleiman.