Mchekeshaji ajulikanae kwa
jina la kisanii wa Nchini Tanzania, Mc Pili Pili akitoa vibwagizo vya
uchekeshaji kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika 1 Agosti 2014 jijini Dar es Salaam
kuhusina na maandalizi la onesho la vichekesho litakalofanyika kesho Agosti
2,2014 katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam wa pili kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis,ambaye ndio
waandaaji wa Onesho hilo, Mchekeshaji kutoka
nchini Uganda,Anne Kansiime (wa pili kulia), Kushoto kwake mchekeshaji kutoka
nchini Kenya,Fred Omondi.
Mchekeshaji ajulikanae kwa
jina la kisanii wa Nchini Tanzania, Mc Pili Pili (kushoto), akiwa na mchekeshaji kutoka nchini Kenya,Fred Omondi.
HABARI
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
Mchekeshaji
Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki
wake katika ukumbi wa Golden Tulip.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha
na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo
Jumamosi.
‘Hii ni mara
yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo
itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi
kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.
Kwa upande
wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema
watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka
Kwa Nguvu.
‘Usiku wa
Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo
watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.
Naye
mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa
kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka
Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya
muziki kutoka ODAMA Band.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka
wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani
waliyowaandalia. ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia
Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema
Robert.
Kansiime
amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande
vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto
mbalimbali za maisha.
Mchekeshaji
huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime”
kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee
nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.

