| Waziri wa vijana utamaduni na Michezo akiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya TSN ,Ndg Farough Baghoza wakishuka katka ndege ya Fastjet katika uwanja wa kimaTaifa Kimanjaro/KIA wakiwa na Wachezaji Wa Real Madrid ya Hispani,Tsn ndio waliowezesha kuja kwa Timu hiyo ambayo nifaida kubwa kwa nchi yetu.Tsn imekuwa mstali wa mbele katika kutoa misa-ada hapa nchini ingawa haijitangazi katika vyombo vya habari,Tsn ikishilikiana na kampuni ya Homeshoping center ilifanikisha ujenzi wa Hospital,Kituo cha Polisi,na shule Mabwe Pande makazi mapya kwa watu waliopatwa na mafuliko na nyumba zao kusombwa na maji ,lilikuwa ni janga la kitaifa. | |
ni vizuli kwa jamii kuwathamini na kuwatambua waTanzania ambao wamekuwa mstali wa mbele katika kuchangia maendeleo nchini.
ENDELEA KUFUATILIA PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO.
IMEANDALIWA NA Bernard James wa www.mtazamomedia.blogspot.com
+255752106535
..........................
IMEANDALIWA NA Bernard James wa www.mtazamomedia.blogspot.com
+255752106535
..........................
Baadhi
ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid wakiwasili katika uwanja wa
Ndege wa KIA .
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Panone Ltd Patrick Ngiloi akisalimiana na mmoja wa wageni
waliokuwa wameambatana na ugeni huo.
Ugeni toka klabu ya
Real Madrid ukiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA.)
Magwiji
hao walipokelewa na ngoma ya asili kutoka kikundi cha Msanja cha mjini Moshi.
| Magwiji hao walikabidhiwa Maua uwanjani hapo kama ishara ya Upendo kwao. |
Mkurugenzi
wa Panone Ltd,Patrick Ngiloi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa TSN
,FarouK Baghoza mara baada ya kupokea ugeni toka Real Madrid.
Ugeni
wa Real Madrid ukiwasili katika hotel ya Panone Luxury Motel iliyopo King'ori
jijini Arusha.
Mkangara
akiongozana na mkuu wa wilaya ya Rombo ,Elinasi Parangyo kusindikiza Ugeni toka
Real Madrid.
Viongozi wa
serikali wakipata viburudisho.
Wachezaji
wa Real Madrid wakiteremka toka katika basi wakiingia hotel ya Panone Luxury
Motel kwa jaili ya viburudisho.
Friends Of Panone wakiwa katika picha ya Pamoja na magwiji hao.
Kikosi cha Machava fc .
Kikosi cha Panone fc.
Kikosi cha wachezaji wa zamani waklabu ya Real Madrid kikiasili katika uwanja wa Ushirika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwapokea wageni hao.
Wachezaji wa Real Madrid wakiteremka toka katika basi wakiingia hotel ya Panone Luxury Motel kwa jaili ya viburudisho.
Wageni wakijiandaa kusalimia vikosi vya Panone fc na Machava fc.