Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Mama Mary Mbaga Makame, mjane wa
Marehemu Jaji Lewis Mhina Makame mara baada ya kuwasili kijijini Tongwe,
wilayani Muheza kwa ajili ya mazishi
tarehe 23.8.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiaga mwili wa Marehemu Jaji Lewis Makame kijijini
kwake huko Tongwe, wilayani Muheza tarehe 23.8.2014.
Mama Salma
Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva muda
mfupi kabla ya kuanza ibada ya mazishi ya Marehemu Jaji Lewis Makame
iliyofanyika katika Kanisa Anglikana la
Mtakatifu Yusuf huko Tongwe, wilayani Muheza.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akifuatana na Mama Mary Makame, mjane wa Marehemu Jaji Lewis
Makame kuelekea kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa Anglikana
Tongwe huko Wilayani muheza tarehe 23.8.2014.
Mama Salma
Kikwete akifuatana na Mama Mary Makame na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Mheshimiwa Angela Kairuki (kwa kwanza kulia) wakielekea kanisani.
Waombolezaji wakiingiza kanisani jeneza lenye mwili wa Marehemu Jaji Lewis Makame kwa ajili ya misa ya ibada maalum.
Waombolezaji wakiwa Kanisani
Mama Salma Kikwete akitoa neno la faraja kwa
wafiwa mwishoni mwa ibada ya kumuombea marehemu Jaji Lewis Makame iliyofanyika
katika kanisa Angilkana Tongwe huko Muheza.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiongoza msafara wa mamia ya waombolezaji kwenda makaburini kwa ajili
ya mazishi.
Jaji Mkuu
Mheshimiwa Chande Othman alikuwa ni miongoni mwa majaji wa Mahakama Kuu na
Rufaa waliobeba mwili wa Marehemu Jaji Lewis Makame kuupeleka kwenye nyumba
yake ya milele huko kijijini kwake Tongwe katika wilaya ya Muheza.
Askofu wa
Kanisa Anglikana Dayosisi ya Tanga Dr. Williama Mndolwa akiwaongoza maaskofu,
makasisi na mashemasi kuweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Jaji Lewis
Makame.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akimsindikiza Mjane wa Marehemu Jaji Lewis Makame, Mama Mary
Makame kuweka udongo kwenye kaburi.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi .
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete na Mama Mary Makame wakiwa na nyuso za huzuni wakati wakishuhudia shughuli ya utiaji
udongo kaburini.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akitoa salamu ya pole kwa wafiwa mara baada ya shughuli ya
utiaji udongo kaburini kukamilika.
Mjane wa
Marehemu Jaji Lewis Makame, Mama Mary akiweka shada la maua kwenye kaburi la
mume wake Marehemu Jaji Lewis Makame wakati nwa ibada ya mazishi iliyofanyika
huko Tongwe katika wilaya ya Muheza tarehe 23.8. 2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka shada la
maua kwenye kaburi la hayati Jaji Lewis Makame wakati wa mazishi yaliyofanyika
katika kijiji cha Tongwe katika wilaya ya Muheza, mkoani Tanga tarehe 23.8.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI