Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya
Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na
Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli
za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman
Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi
na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo.
(PICHA NA
KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKURANGA -PWANI)
Mbunge
wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama
Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi wa
kata ya Kimanzichana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini
hapo leo Mkuu wa Wilaya ya
Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara leo.
Baadhi ya wananchi
wakipunga mikono kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo
pichani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kimanzichana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia
mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano mjini
Kimanzichana, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli ya
kufyatua matofali pamoja na wanakikundi wa kikundi cha Mkuranga Youth
Development ambapo amekipa kikundi hicho mashine 2 ili kuongeza uwezo wa
kikundi hicho.
Mmoja
wa wanakikundi wa kikundi cha Mkuranga Youth Development Bi Faraja
Msani akionyesha jinsi wanavhoshiriki shughuli za kujiletea maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli ya ujenzi wa mafarasa katika shule ya sekondari ya Mwarusembe huku wananchi wakiendelea na kazi ya kukusanya matofali.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mwarusembe.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani kutoka Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akionyesha ripoti
mbalimbali za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM wakati wa kutano
wa ndani na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Pwani.
Mmoja wa viongozi wa CCM wilayani Mkuranga Bi Agricola akiwa katika mkutano huo