Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias.Marion Elias (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Septemba 30,2014 jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maonesho ya utengenezaji Keki "Azam World Of Cakes Exhibition" yanayotarajiwa kufanyika 6,Disemba 2014 katika Hoteli ya Serena (katikati) ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma Kampuni ya Bakhresa Group-Azam,Mohammed Ramadhani (kushoto), Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias.Marion Elias (kulia), akiteta jambo na Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma Kampuni ya Bakhresa Group-Azam,Mohammed Ramadhani wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria kwenye mkutano huo.
Habari/Picha na Philemon Solomon
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Insight Consultants.Marion Elias alisema maonesho hayo yatawakutanisha wadau mbalimbali wa makampuni na taasisi waandaji wa keki nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shghuli.
Alisema dhumuni la maonesho hayo ni kusherekea taaluma ya ukokaji keki na kuonesha ubunifu na utaalam wa utengenezaji na urembaji keki.Alisema washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha bidhaa zao za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya utengenezaji bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao.
Pia alisema maonesho mengine yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na uhifadhi bora wa keki kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki kuonesha maumbo mbalimbali ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na jamii nzima.
Alisema maonesho hayo yanadhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hiyo yatawashindanisha wadau wa uandaaji keki na washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho watajipatia fedha taslimu na bidhaa mbalimbali.
"Hili onesho litahusisha jamii yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki, upambaji wa keki, wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa mbalimbali zinazotumika kutengenezea keki kama vile unga wa ngano wa Azam" Alisema Elias.
Pia onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli mbalimbali vyuo vyao taaluma ya hoteli hapa nchini na majirani kutoka Afrika Mashariki pamoja na watengenezaji keki binafsi.Wananchi watakaotembelea maonesho hayo ambao hayata kuwa na kiingilio watapata furusa ya kujionea aina na mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki pamoja na kuonja bidhaa hiyo kwenye maonesho ambayo.ambayo yatafanyika katika hoteli ya Serena Desemba 6,2014 jijini Dar es Salaam.
Angalia picha mbalimbali za keki.













0 Comments