MONROVIA-Liberia watu wengi wameambukizwa virusi vya ugonjwa
wa Ebola na wengi wao wapo katika hali mbaya,magari ya wagonjwa ambulance
yamekuwa yakichukua wagonjwa na kuwapeleka katika zahanati za katikati,
Hali ni mbaya na imemlazimu Rais kuiomba Marekani itume
vikosi ya matibabu ilikukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao unatishia uhai wa
wariberia na kuliteketeza Taifa.Rais anasema misaada zaidi inahitajika ,Rais
Ellen Johnson Sirleaf jumatano hii
ameiomba jumuiya ya kimataifa kuzidisha misaada mala 2 ilikukabiliana na
ugonjwa huu,ambao unaenea kwa kasi sana.
Kuna hatari ugojwa wa ebola kusambaa katika mataifa mengine
za Afrika,baada ya kuwa tayari umeisha
shambulia mataifa matano ya Afrika magharibi.
Marekani ni wenzetu hapa Liberia,atuwezi peke yetu katika
kuutokomeza ugonjwa huu alisema Sirleaf katika taarifa yake
iliyosomwa,tunatumaini uamuzi wa Marekani utachochea jamii ya kimataifa kuchukua hatua ya kuungana ilikuutokomeza ugonjwa wa
ebola,wafanyakazi wengi wa afya waliokuwa wanahudumia wagonjwa ,wengi wao
wamegunduliwa kuambukizwa ,katika nchi za Guinea,Liberia na Siera leoni nusu
yao tayari wamekufa,pia wafanyakazi wa afya kutoka ulaya walioenda kusaidia
ambao wako saba wamegundulika kuwa na vijidudu vya ebola na tayali wamepelekwa
katika nchi za ulaya kwa matibabu wakiwa chini ya uangalizi,
Imekuwa vigumu sasa kuwapa mafunzo wahudumu wengine wa afya
kwa ajili ya kwenda kutoa hudma katika nchi hizo kutokana na maambukizi
yalivyo.,kunamlipuko mkubwa wa ugonjwa wa ebola.
