Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO),
Meekson Mambo.
Makamu wa Rais IMTUSO. Walter Nnko
Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU,
Benson Lukwambe. Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na
Teknolojia IMTU (IMTUSO), (katikati), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma
kufuatia maagizo ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) dhidi ya chuo cha
IMTU. Kulia ni Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson
Lukwambe na Makamu wa Rais, Walter Nnko.
Dotto Mwaibale
WANAFUNZI
wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU wameiomba Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuunda tume maalumu itakayoshirikisha
uongozi wa wanafunzi kufuatia utekelezaji wa maagizo waliyokiwekea chuo
hicho ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Rais wa Serikali ya wanafunzi
wa chuo hicho,IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo alisema wanafunzi wa chuo
hicho wana wasiwasi kuhusiana na muda wa miezi mitatu uliotolewa na TCU
kuhakikisha chuo cha IMTU kimekamilisha masharti yote waliyopewa
vinginevyo kitafungwa.
“Matatizo
ya chuo hicho ni ya muda mrefu hivyo kukiwa na kamati maalumu itasaidia
kushughulikia suala hilo haraka na kulitafutia ufumbuzi badala ya
kukifunga chuo hicho ambako kutaleta athari kubwa katika masomo kwa
wanafunzi” alisema Mambo.
Mambo
alisema TCU iunde kamati ya muda itakayoshirikiana na uongozi wa chuo
uliopo sasa pamoja na uongozi wa wanafunzi waweze kusimamia na
kuhakikisha kuwa maagizo ya TCU yanatekelezwa ili kutoa fursa kwa
wanafunzi kuendelea na masomo huku mapungufu ya muda mrefu yaliyopo
yakiendelea kutatuliwa kwani muda huo wa miezi mitatu waliopewa ni
mdogo.
Aliongeza
kuwa endapo uongozi wa chuo utashindwa kutekeleza maagizo ya TCU
hawaungi mkono hoja ya kufunga chuo badala yake kiwekwe chini ya
serikali au chuo kikuu kingine ambacho kina kitakuwa na uwezo wa
kusimamia mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaa ambacho hakina kitivo cha
afya.
Makamu
wa Rais wa Serikali ya chuo hicho, WalterNnko alisema kukifunga chuo
hicho kutawaathiri wanafunzi zaidi ya 1000 waliopo chuoni hapo.
0 Comments