Random Posts

SITTA NA FREDERICK WAREMA NI MAADUI WAKUBWA WA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA NA BORA YA TANZANIA_JUKATA



 Na Bernard James      0652152000
Jukwaa la katiba Tanzania (Jukata)limemtangaza Mhe Samweli Sitta ambae ni mbunge wa jimbo la urambo na Spika wa bunge maalumu la kuandika katiba mpya ,pamoja na Mwanasheria mkuu wa Serikali jaji Warema kuwa ni maadui wakubwa wa upatikanaji wa katiba bora ya Tanzania,
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa jukata ,Deus M Kibamba  alisema Mwanasheria mkuu wa serikali na Sitta wanawapotosha kwa makusudi wabunge wa waliopo Dodoma kuwa katiba mpya itapatikana hata bila kuwepo Ukawa,na mwanasheria mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wanajuwa haiwezekani ,Kupatikana katiba bila malidhiano,Kibamba a lienda mbali zaidi na kusema kuendelea kwa mchakato Dodoma kwasasa ni ufujaji wa pesa za waTanzania walipakodi kwa manufaa binafisi sio kwa ajili ya manufaa ya wa Tanzania,ameshauli kusitishwa kwa bunge mala moja ,
Jukwaa la katiba la Tanzania lilipokea kwa furaha tamko la vyama vya siasa lililotokana na makubaliano yaliofikiwa kwenye mkutano kati ya vyama vya siasa vilivyo chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)na Mhe Rais iliyofanyika tarehe30/8/2014 na 8/9/2014 ikulu ndogo ya chamwino Dodoma,kutokana na mazungumzo hayo,ilikubaliwa mchakato wa katiba mpya uairishwe hadi  baada ya uchaguzi wa 2015
Deus alisema Bunge maalum la katiba (bmk)limekosa uhalali wa kisiasa kutokana na kutoka nje ya bunge kwa kundi la UKAWA na mahudhulio duni kutokana na mahudhulio duni kutokana na wabunge 25 wa CCM kutoshiriki vikaotangu bunge lilipoanza Agosti05/2014
Bunge pia limekosa uhalali wa kisheria itakapo kuja kwenye kupata2/3 kutoka Zanzibar wakati wakupigia kura vifungu na ibara mbalimbali za katiba,kwa hiyo kuendelea na  bunge la katiba ni  kuendeleza wizi wa mabilioni ya waTanzania na ufujaji na kufuru ya matumizi ya fedha za umma za walipakodi waTanzania ambao ni masikini.kujiengua kwa mwanasheria  mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Othumani Masoud Othumani kutoka katika kamati ya uandishi ya bunge maalum la katiba kumekuwa ni pigo kubwa kwa mchakato wa katiba mpya na hususani bunge maalum .habari ya kuwa kuondoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar hakuna pengo lolote kama Sitta na Warema wanavyotaka kuaminisha jamii,ni propaganda na upotoshaji unaostahili kupuuzwa ikizingatiwa kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar ndie kiongozi wa jopo la waandishi na wanasheria  kutoka upande wa Zanzibar na mshauri mkuu  wa sheria wa SMZ.kwa hiyo kujiengua kwake ni pigo kubwa na athali kwa
maslai ya Zanzibar,Deus Kibamba amewaomba waTanzania kwa ujumla wake kumuona Mhe Samweli Sitta na Mwanasheria wa Serikali Jaji Warema kuwa ni maadui wakubwa katika kupatikana kwa katiba bora kwa masilai ya Tanzania na vizazi vijavyo,kwa hiyo wasipewe nafasi yeyote  katika chaguzi zijazo kwa muda wa miaka kumi 10 iliwajirudi,na mchakato unaoendelea hivi sasa kule Dodoma ni masilahi binafisi, na usitishwe malamoja alisema mwenyekiti Deus