Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akiteta jambo
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Afande Leonard Paul, wakati wa
chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya wachezaji
wa timu ya polisi mkoani Morogoro na wajumbe wa idara ya utumishi wa
walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo
mkoani Morogoro, Alhamisi Oktoba 23, 2014.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisalimiana na baadhi
ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, Jumatano Oktoba 22, 2014,
wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wachezaji
hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya
siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza na wajumbe
wa idara ya utumishi wa walimu, wakati wa chakula cha usiku
kilichoandaliwa na Mfuko huo mjini Morogoro Oktoba 22, 2014. Wajumbe hao
wanatarajiwa kubhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo
ili kuwaelimisha walimu faida wanazoweza kupata endapo watajiunga na
Mfuko huo.
Meneja
wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa
Seme, akiwasalimia walimu ambao ni wajumbe kutoka idara ya utumishi wa
walimu wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa wajumbe hao
wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF, ili kuelezea
shughuli mbaklimbali na faida unazoweza kupata unapojiunga na Mfuko huo.
Semina hiyo ilifanyika mkoani Morogoro
Msanii
Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo, wakati wa
chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya
utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na
Mfuko huo mkoani Morogoro. Picha na Masogange
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 Comments