Vyeti vya ushindi
Na Matukiodaima Blog
KAMPUNI
ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa mara ya nne mfululizo imeendelea
kushika nafasi ya kwanza kitaifa uzalishaji wa maziwa nchini
.
Kampuni hiyo imeshinda tuzo ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa bora za maziwa
katika mashindano wiki ya maziwa yaliyofanyika juzi kwenye viwanja
vya shule ya sekondari Mpechi mkoani
Njombe .
Kampuni hiyo imeibuka
mshindi wa kwanza
baada ya kuongoza katika nafasi zote tatu
za ubora wa
bidhaa zilizoshindanishwa katika
mashindano hayo .
Akikabidhi tuzo hizo Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo pamoja na
kupongeza makampuni yaliyoshiriki katika zoezi hilo bado alipongeza kampuni ya Asas Dairies Ltd kwa
kufanya vizuri katika mashindano hayo ya ubora wa maziwa
nchini
Alisema kuwa jitihada zilizoonyeshwa na kampuni hiyo ni
kubwa na zinapaswa kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.
Kwani alisema kuwa kuongoza katika nafasi
zote zilizoshindaniwa si jambo dogo
ni jitihada kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni
hiyo.
Pia aliipongeza bodi ya maziwa
Tanzania kwa kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya kipimo
kwa wamiliki wa viwanda vya maziwa nchini na sehemu ya
kujitathimini .
Kwa upande wake
meneja uzalishaji wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Lipita Mtimila alisema kuwa mbali ya
kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu bado ilipata
kuongoza katika mashinadano kama haya miaka mitatu
nyuma na hii ni mara ya nne kuongoza .
Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa
Tanzania( TDB) kampuni ya Asas Dairies
iliweza kuibuka na ushindi wa jumla baada ya kushinda tuzo
zote tatu dhidi ya makapuni
mengine ya uzalishaji maziwa yaliyoshiriki katika mashindano hayo .
Bw Mtimila aliwataka
watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd
na kuwa
lengo la kampuni hiyo ni
kuendelea kuzalishaji bidhaa zenye ubora zaidi .
Pia alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies
Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa kuendelea
kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa
|