Random Posts

WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Christina Mndeme akiwasha Mwenge wa uhuru katika mnara wa mashujaa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mshujaa, hafla iliyofanyika Saa Sita Kamili usiku ya tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Jordan Rugimbana akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuupa heshima Mkoa wa Dodoma wa kuadhimisha siku ya mashujaa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kutoa rai kwa watanzania kuwa wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya mtu kama walivyofanya wazee wetu waliopigania uhuru wa nchi.

Wanajeshi wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwashwa kwa Mwenge kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mshujaa yatakayofanyika tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.