Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu
Chiku Galawa (Kulia) akitoa maelezo ya hali ya miundombinu ya mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea ofisini kwake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia) wakati alipotembelea ofisini kwake kupata
taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa huo.
Meneja wa wakala wa barabara nchini
(Tanroads) mkoa wa Mbeya Eng. Paul
Lyakurwa (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu barabara ya Ikana-Makamba
–Chitete kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa
kwanza kushoto) wakati alipokagua barabara hiyo kwenye mkoa wa Songwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa wakala wa
barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa wakati alipokagua
barabara ya Ikana-Makamba –Chitete iliyopo mkoa wa Songwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua kituo cha kukuza mawimbi ampilification station kilichopo
miangalau mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Meneja wa kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) Mkoa wa Katavi na Rukwa Bw. Peter Kaguru.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen
akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu katika mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipomtembelea ofisini
kwake.
Meneja wa Wakala wa barabara nchini
(Tanroads) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa pili kushoto) akisoma taarifa ya
utendaji ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kwa Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa
taasisi hizo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa
taasisi zilizo chini ya yake (hawapo pichani), wakati alipokutana nao Mkoani
humo.
Viongozi wa taasisi zilizo chini ya
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoani Rukwa, wakimsikiliza Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani)
wakati alipokutana nao Mkoani Rukwa.
.......................................................................................................
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara
yake kuanzisha mfumo maalumu wa makubaliano utakaotumika kupima utendaji kazi
wa watumishi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutoa matokeo chanya.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo Mkoani
Rukwa alipofanya mazungumzo na Viongozi na watendaji wa taasisi hizo wakati
alipotembelea mkoa huo kwa lengo la kukagua hali ya miundombinu na kuwaeleza
mtazamo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema katika mfumo huo Waziri
ataingia mkataba na wenyeviti wa bodi wakati Katibu Mkuu wa kila sekta kuingia
mkataba na watendaji wakuu wa taasisi hizo na watendaji hao wataingia mikataba
na wafanyakazi wao ili kuweza kuweka mazingira ya kila mfanyakazi kufikia
malengo yaliyowekwa na wizara pamoja na taasisi husika.
“Mimi nitawekeana mkataba na wenyeviti
wa bodi za taasisi zote, kwa Sumatra moja ya vipengele vitakavyokuwa
kwenye mkataba huo ni pamoja na mkakati
madhubuti wa kupunguza ajali za
barabarani zinazosababisha vifo kwa
Watanzania, TCRA Makusanyo kwenye makampuni ya simu na taaasisi nyingine hivyo
hivyo”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Waziri Mbarawa amehimiza
taasisi hizo kufanya kazi kwa bidii ili kuwajengea miundombinu iliyo bora
watanzania ili kuweza kuwafikisha katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Aidha, Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao
kufanya kazi kwa ubunifu, kasi na uadilifu ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na
kuwajibika kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kubadili maisha ya watanzania
kwa ujumla.
“Ni wakati wa kutekeleza kauli mbiu ya
hapa kazi tu kwa vitendo, hivyo nawataka muwe wabunifu katika utendaji kazi za
kila siku na muweze kutoa matokeo chanya ya haraka kwa wananchi”, amesisitiza
Prof. Mbarawa.
Awali akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa, Profesa Mbarawa amesema Serikali kupitia
wizara yake itaendelea kupandisha hadhi baadhi ya barabara zilizo chini ya
Halmashauri na kuwa chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), ili kuweza
kuendelea kuboresha hali ya miundombinu na kuunganisha mkoa huo na Mikoa ya
Mbeya, Rukwa pamoja na nchi zinazozunguka mikoa hiyo kwa barabara za lami.
Profesa Mbarawa amemuhakikishia Mkuu
wa Mkoa huyo kuwa Serikali itaendelea kufanya matengenezo kwa barabara zote
nchini kupitia gawio kutoka Mfuko wa Barabara nchini (Road fund) ili kuinua
uchumi wa Mkoa.
Waziri Mbarawa yupo katika ziara ya
kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi pamoja na hali ya Miundombinu katika mikoa
ya nyanda za juu kusini.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.








