Mwonekano wa Zahanati Mwendo kwa nje
Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo
Madereva wakipima afya zao.
........................................................................................
Huduma ya Zahanati Mwendo ambayo imebuniwa na kampuni ya TBL
Group katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani kwa ajili ya
kupima afya za madereva imekuwa kivutio kikubwa mkoani Geita ambako maadhimisho
haya yamezinduliwa kitaifa na idadi kubwa ya madereva na wananchi wanaendelea
kujitokeza kupima afya zao kwa wingi na kupatiwa matibabu na ushauri nasaha.
Madaktari maalumu waliopo kwenye gari la kufanyia vipimo la
Zahanati Mwendo muda wote tangia kuwasili mkoani Geita wamekuwa na kazi kubwa ya kutoa huduma kwa madereva wengi na wanaendelea
kujitokeza kufanyiwa vipimo siku hadi siku.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group ,Amanda Walter,amesema inavutia kuona watanzania wengi wanahitaji
huduma ya kupimwa afya na kumekuwepo na
mwitikio mkubwa wa madereva na wananchi wanaotembelea Zahanati Mwendo.
Alisema pia kuwa wananchi wengi wamejitokeza katika semina
ya Mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu yaliyofanyika katika kituo Kikuu cha mabasi
cha Geita ambapo walipata fursa ya kujua madhara ya matumizi ya vinywaji vyenye
kilevi kupindukia.
''Wiki ya Usalama ya mwaka huu imekuwa na mwamko mkubwa
hususani wananchi walivyojitokeza kwa wingi katika mafunzo haya ya Unywaji wa
Kistaarabu na mengine yanayohusina na Usalama barabarani.TBL Group tunaendelea
kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kampeni za Usalama kwa lengo
la kupunguza matukio ya ajali nchini”Alisema.
Rehema Nyoki,mkazi wa Geita ambaye amehudhuria mafunzo ya
Unywaji wa Kistaarabu akiongea kwa niaba ya wenzake aliipongeza kampuni ya TBL
Group kwa kuendesha semina za uhamasishaji unywaji kistaarabu na alitoa ombi mafunzo hayo yafikishwe sehemu mbalimbali
nchini kwa kuwa ipo idadi ya waathirika wengi wa kutumia vinywaji vyenye kilevi
kupita kiasi kwenye jamii ambao
wanaishia kupata matatizo ya kila aina.




0 Comments