![]() |
| Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo septemba 16, 2016. |
Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa.
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali
hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya mashine ya MRI kuanza
kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Joshua Job na
Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa hospitali hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika kwenye hospitali
hiyo.
Picha na John
Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
..........................................................................................
Na
John Stephen, MNH
Dar
es Salaam, Tanzania. Mashine ya MRI katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) imepona baada ya kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine
hiyo iliharibiika baada ya kutokea
hitilafu ya umeme. Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52 wamepatiwa
kipimo cha MRI.
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare
amesema baada ya mashine hiyo kuharibiika, mafundi wa Philips kwa kushirikiana na
mafundi wa Muhimbili walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza
ufanisi katika mashine hiyo.
“Tarehe
26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza
ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda
mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module
kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza
kifaa hicho kutoka Uholanzi,” amesema Dk Lwakatare.
Mmoja
wa ndugu wa wagonjwa, Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba tangu
kuharibiika kwa mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi baada ya
kurejea kwa huduma hiyo.
“Tunashukuru
huduma za MRI zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni nafuu kuliko kuliko
kupata matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza madaktari na wauguzi kwa
utendaji bora.
Naye
Hawa Hussein mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa.
Hawa
ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za kuiwezesha mashine
hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa.
Amesema
kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana imani wataendelea
kupata huduma bora na kwa wakati.




0 Comments