Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi
Gerson Lwenge akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali itahkikisha
inaipa kipaumbele miradi ya maji ambayo haikutekelezwa kwa awamu ya kwanza,
wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdalah Ulega (katikati)akiwaeleza
jambo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. James Mbatia
akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu
Nchemba akijibu swali Bungeni na kuwataka wananchi kufuata kanuni sheria na
taratibu za nchi, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter
Muhongo akijibu swali wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa akilihutubia Bunge kabla ya kutoa kauli ya kuliahirisha
bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016 ambapo mbali na mambo mengine amesema
serikali itaendelea kutekeleza yale iliyoyaahidi na kuwashukuru wadau
mbalimbali wanaoendelea kujitolea kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiimba
wimbo wa taifa baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1
Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya Waziri Mkuu
kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakibadishana mawazo na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa baada ya
kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiteta jambo na Mbunge
wa Jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea, baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge
hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO











0 Comments