Venance Mwamoto
.................................................................................................................
Na Matukiodaima Blog
KOCHA wa timu ya Bunge Venance Mwamoto ametoa mwaliko kwa timu ya
Bodaboda kilolo kwenda bungeni kucheza mchezo wa kirafiki na wabunge
Mwamoto
ambae ni mbunge wa Kilolo mkoani Iringa alitoa mwaliko huo wakati wa
kikao chake na vijana hao wa bodaboda mjini Ilula Jana.
Alisema
kuwa kabla ya kwenda bungeni vijana hao watashindana kupata bingwa wa
mashindano hayo ambaye atakwenda Dodoma kucheza na wabunge
Hivyo alisema lazima kujipanga vema kwa kujiandaa ili kuepuka aibu ya kichapo kutoka kwa wabunge.
"Nawaomba
timu itakayoshinda iwe bungeni kutangaza wilaya getu ya Kilolo kisoka
pia kuanza rasmi kwa mashindano ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia
Abdalah na mimi mbunge wenu nitadhamini "
Hata hivyo alisema
kabla ya mashindano hayo atatoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki
kama njia ya kuondoka kero ya vifaa vya michezo.
Mwamoto alisema
lango ni kuona vijana Kilolo wanakuwa na timu na kupitia michezo
wanapata ajira kwa kuchezea timu mbali mbali kubwa nchini. |