
![]() |
![]() |
Mbunge Ridhiwani akizungumza na waandishi wa habari
hawapo pichani katika ufungaji wa mafunzo ya usalama wa barabarani kwa waendesha
bodaboda wa Wilaya ya Chalinze
|
![]() |
| Baadhi ya vijana waliofuzu mafunzo na kupatiwa leseni ya udereva wa bodaboda msaada wa Ofisi ya Mbunge wa Chalinze wakifuatilia kwa makini yanayotokea katika kikao hicho |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ameshirikiana na Gsm Foundation na MOI kusaidia
kutibu watoto nane wenye matatizo ya vichwa
vikubwa na mgongo wazi.
Katika matibabu hayo watoto
wapatao 23 walifanyiwa vipimo na 8 kati yao walikutwa na matiatizo hayo na
kufanyiwa upasuaji,na kuongeza kuwa watoto wengine walikutwa na matatizo
tofauti na hayo,na kupelekwa katika hosptali ya taifa Muhimbili na wengine
walipelekwa kwa madaktari bingwa wa magonjwa kwa matibabu.
“Watoto wote
waliofanyiwa operesheni tuliwakuta wanaendelea vizuri wakiwa na wazazi wao
wakiendelea kuwapatia huduma za mwisho kabla ya kuruhusiwa”,alisema Kikwete
Aidha,Mbunge huyo
amewaomba wazazi kutowaficha watoto wenye matatizo kama hayo kwani yanatibika
na kuacha kuendekeza Imani potofu za kuwafungia ndani na badala yake kuwapeleka
katika vituoa vya afya ili kupata matibabu.
“Nawashauri wazazi
kutowafungia ndani watoto wenye matatizo kwa kufanya hivyo ni kuwanyima watoto
nafasi ya kupona na kuishi maisha kama watoto wengine”,alisema Kikwete.
Kikwete amewaomba wadau
katika sekata ya afya kujitokeza kuungana na Gsm Foundation katika kusaidia
katika sekta hiyo ili kumkomboa mtanzania kuondoka na matatizo ya kiafya
yanayowakabili.
“Nawashukuru sana Gsm
kwa kujitoa kusadia watoto hawa kupata matibabu kwa ni jambo la kupigiwa mfano
na wadau wengine katika kusaidia jamii”,alisema Kikwete
Mbunge huyo ameshukuru
madaktari kwa kujitolea muda wao na kuwatibu watoto hao na kutoa wito kwa Gsm
Foundation kuondelea kusaidia katika Mkoa wa Pwani ili kuwafikia watoto wengine
katika maeneo ya Mkuranga,Kibiti,Mafia na Rufiji.
Katika hatua nyingine Ofisi
ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa polisi Mkoa
wa Pwani,polisi Wilaya ya Chalinze na kituo cha udereva wa vyombo vya moto cha
Winners Driving School wameendesha
mafunzo ya udereva kwa vijana 160.
Mafunzo hayo ya udereva yamewezesha vijana hao kupatiwa
leseni mara baada yakumaliza mafunzo yatakayo wasaidia katika shughuli zao za
kila siku za kujitafutia kipato,mafunzo hayo yamegharimu shilingi milioni 20.






0 Comments