Aliagiza Baraza lifanye Operesheni ya kuhakiki
Vyeti vya Wataalam wa Dawa (Wafamasia) nchi mzima ili kuthibiti Wauza Dawa Feki.
Alitaka kuwafutia usajili wafamasia wanaouza
Dawa za Serikali"
Na.Mwandishi Wetu - Dodoma.
9/9/2016.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Famasia nchini
kuanza kazi ya uhakiki wa vyeti vya wauza dawa katika maeneo mbalimbali nchini
kwa lengo la kudhibiti na kuwaondoa wauza Dawa wote wasio na sifa ya kufanya
kazi hiyo.
Pia ameligiza Baraza hilo kuwachukulia hatua
kali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kuwafutia usajili wafamasia wanaokiuka
kanuni na taratibu za Baraza hilo ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya
upotevu wa dawa, vifaa na Vifaa Tiba vya Serikali.
Mhe.Ummy aliyasema hayo jana mjini
Dodoma katika Kikao Chake cha kwanza na Bodi ya Baraza la Wafamasia nchini
ambapo pamoja na mambo mengine alikemea utaratibu ulojitokeza hivi karibuni wa kutaka kuifanya biashara ya
dawa kuwa sawa na biashara nyingine za kawaida za maduka ya kuuza nguo jambo
ambalo halikubaliki.
"Biashara ya maduka ya dawa lazima
iheshimiwe, lazima ianzishwe kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja
na watu wanaoajiliwa kuhudumia maduka ya dawa kuwa na sifa zinazotakiwa, kazi
ya kuuza dawa za binadamu sio sawa na biashara ya kuuza nguo au viatu",
alisema Mhe Ummy....
Ameliagiza Baraza hilo kufanya operesheni nchi nzima kukagua maduka yote ya dawa kubaini mapungufu
yaliyopo kisha kuchukua hatua kali dhidi ya wale wataogundulika kufanya
biashara hiyo bila kufuata taratibu na kuongeza kuwa baraza hilo ni lazima
liendelee kupambana na watoa dawa wasio na sifa
na wale wasio waaminifu wanaotengeneza vyeti bandia vya Wataalam wa Famasi.
Pia ametoa maelekezo kwa baraza hilo kuangalia suala la mgongano wa maslahi hasa
pale ambapo Mfamasia wa Wilaya anatuhumiwa kumiliki maduka ya Dawa mawili hadi
matatu ndani ya Halmashauri anayofanyia kazi.
"Ni lazima suala hili
tulitafutue suluhish nimefanya ziara mikoani jambo hili nimelikuta, mimi
sielewi na Wananchi wengi hawaelewi pale Mfamasia wa Wilaya anapokua na maduka
ya dawa hadi matatu na muda wote yana
dawa wakati dawa hizo hizo hazipatikani katika vituo na Hospitali za Serikal, Kwa
nini wananchi wasiwe na hisia kuwa dawa zile ni za Serikali? Baraza nileteeni
mapendekezo ya kutatua hili. Alisisitiza Mhe Ummy.
Aidha, ameliagiza Baraza hilo kuweka msukumo wa pekee
kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili nchi iwe na wanataaluma wenye
uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu.
Akitoa Taarifa ya Utendaji Msajili wa
Baraza la Famasia Bi.Elizabeth Shekalaghe alieleza kuwa zipo changamoto
wà nazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo maduka mengi ya kuuza
dawa kuendesha biashara hiyo bila ya kuwa na vibali vya biashaa pia kuwepo kwa
wauza dawa wasio na sifa ya kufanya shuguli hiyo.
Pia alieleza mikakati iliyowekwa na
barza hilo ili kuhakisha changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi ili
kuhakikisha huduma za uuzaji dawa zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu
ili kuhakikisha unora wa huduma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya
Bà raza là Famasia, Legu Ramadhani Mhangwa, amesema kuwa Baraza hilo limekuwa
likifanya kazi zake kwa kuzingatia
sheria ili kufikia malengo liliyojiwekea na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa
na Mhe Waziri pia kutatua changamoto ya
uwepo wa vyuo binafsi vinavyofundisha taaluma ya famasi kutokidhi viwango
pamoja na nia ya serikali ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kada za dawa
nchini. Pia Baraza limeahidi kushughulikia uhaba wa wakufunzi mahususi katika
vyuo vinavyofundisha kada za famasi katika ngazi ya cheti na diploma.
Kuhusu Mgongano wa maslahi kwa
watumishi wakiwemo watendaji wa Halmashauri na wale wanaosimamia na kutekeleza
kazi za baraza katika ngazi za mikoa na halmashauri, Mwenyekiti huyo ameahidi
kuwa Baraza litahakikisha linasimamia kikamilifu Kanuni za Maadili na Miiko ya
Kitaalamu za 2015 ili kutatua changamoto hizo iliwemo upotevu wa dawa za
Serikali.
