Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey D.J Mwanri,
akitoa soma la fursa kwa baadhi ya Wananchi wake waliyojitokeza ndani ya Ukumi
wa Chuo cha Uwaziri mjini Tabora mapema leo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nikki wa Pili
akiwafungua wakazi wa Tabora kwa kuwaonyesha fursa wanazopaswa kuzitumia ili
waweze kusukuma mbele maendeleo ya mkoa huo.
Msanii wa Muziki wa Kughani Mashairi, Mrisho
Mpoto akiwa amenyanyua mikono juu wakati akiwapa mbinu za mafanikio wakazi wa
Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri (wa nne kutoka kushoto), akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanasemina hiyo.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds
Media Group Ruge Mtahaba (katikati), akiongea jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa huo
wakati akitoa somo la Fursa.
Mkuu wa Chuo cha Mlimani Professional Hassani
Ngoma, akitoa soma la Fursa Ukumbini hapo.
Afisa Masoko wa kanda ya kati wa NMB, Josephine
Kulwa akiwapatia fursa wakazi wa Tabora namna wanavyoweza kufaidika na fursa
mbalimbali kwa kujiunga na baadhi ya huduma zitolewazo na benki hiyo.
Mrisho mpoto akiwa ameketi na baadhi ya watu
waliyohudhulia semina hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Tabora waliohudhulia kwenye
somo la Fursa wakinyoosha mikono kuashiria kuelewa kila wanachofundishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggerey Mwanri, akiagana na Ruge baada ya
kumalidhika kwa Fursa.
.........................................................................................................
MKUU
wa Mkoa wa Tabora MH. Aggrey D.J Mwanri mapema leo alijikuta akitoa ya moyoni
kwa kuisifia kamati na uongozi mzima uliyoandaa tamasha la Fiesta 2016 kwa
kuwapelekea Darasa la Fursa.
Akizungumza
ndani ya Ukumbi wa chuo cha Uwaziri mjini Tabora wakati wa semina hiyo Mkuu wa
Mkoa huo Mh. Aggery Mwanri alisema kuwa, amefurahishwa sana na uongozi mzima wa
Fiesta kwa kuwawezesha wakazi wa mji huo kuwaonyesha namna ya kupambana
kimaisha kwa kutumia rasilimali zilizopo mkoa hapo.
“Napenda
kutumia muda huu kutoa pongezi zangu za dhati kwa waandaaji wa Tamasha la
Fiesta hasa kupitia darasa hili la Fursa ambalo naamini wazi kabisa kila mmoja
wetu aliyehudhulia hapa ataweza kujifunza na kuvuna mbinu mbadala za kujikwamua
kimaisha na kuufanya Mkoa wetu wa Tabora kuongeza uajibikaji,”
Pia
Mh. Mwanra aliwaomba wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya buruda zitakazo
endelea usiku wa leo katika Uwanja wa Ali Hassani Mwinyi kwa kusitarehe na
kuangalia vitu vya msingi vye kuwaongezea kipato zaidi.
Semini
hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds
Media Group Ruge Mutahaba ilionekana kuchangamka vilivyo na kuwafanya baadhi ya
wahudhuliaji wakiwemo wanafunzi wa Chuo hicho kuomba darasa hilo liwe
linawafikia mara kwa mara mjini hapo.













