Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili
Mjini Zanzibar kwa kutumia Boti wakati
alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) alipowasili katika Ofisi za Baraza la
Wawakilishi Zanzibar. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan
Juma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu
Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan
Juma wakati alipowatembelea.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa
tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati
alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na
wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasalimia
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alipotambulishwa wakati wa kikao cha
Baraza hilo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi
Ali Maulid (kulia) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma (kushoto).
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid akimuelezea jambo Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati wa ziara hiyo.
Picha na Ofisi ya Bunge







0 Comments