JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
![]() |
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya
misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti
uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine
katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio
makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Mafanikio
yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA KWA MALI ZA WIZI.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na maafisa wa Polisi wa Mkoa wa Iringa
na Songwe kuanzia tarehe 04.09.2016 hadi 08.09.2016 lilifanya Operesheni ya
pamoja katika mikoa hiyo baada ya watu wasiojulikana mnamo tarehe 07.08.2016
majira ya saa 17:00 jioni kuiba mali iliyokuwa ikisafirishwa ambayo ni sabuni
aina ya Ayu na Duru katoni 4,850 na rangi ya ukutani ndoo 10 aina ya Kale Drdwa za
ujazo wa kilogram 25 na pakiti 08 za rangi ya ukutani aina ya Kale Drdwa zenye
uzito wa Kilogram 15 kila moja. Jumla ya mali yote iliyoibiwa ilikuwa na
thamani ya Tshs. Milioni 69,323,000/=.
Mali
hizo zilizokuwa zikisafirishwa kutokea Dar es Salaam kuelekea Lubumbashi nchini
Kongo na Mfanyabiashara aitwaye CHAPELE
JACKLINE (48) raia wa nchini Kongo.
Katika
Operesheni hiyo maafisa wa Polisi wa Mikoa ya Iringa, Mbeya na Songwe
walifanikiwa kukamata katoni 3,380 pamoja na ndoo 09 za rangi zilizokuwa
zimeibiwa huko Mkoani Iringa eneo la Mavugano Mafinga. Mali hizo zilipatikana
katika mikoa hiyo kama ifuatavyo:-
Mkoani Rukwa
mjini Sumbawanga zilipatikana katoni 240 za sabuni
Mkoani Songwe
katika mji mdogo wa Tunduma zilipatikana katoni 3,100 za sabuni.
Mkoani Mbeya eneo
la Iyunga Viwandani katika Godown zilipatikana katoni 40 za sabuni pamoja na
ndoo 09 za rangi ya ukutani aina ya
Kale Drdwa.
Aidha
katika Operesheni hiyo watuhumiwa watatu walikamatwa kuhusika katika wizi huo
ambao ni:-
1. BOSCO KAMSHA
(52) Mfanyabiashara na Mkazi wa Sae
Mbeya
2.
KENEDY CHISUNGA
(38) Dalali na Mkazi wa Mwanjelwa Mbeya
3.
KENEDY SAMBO
(43) Mjasiriamali na Mkazi wa Manga Veta Mbeya.
Upelelezi
unaendelea ili kuwabaini watu wengine waliohusika katika wizi huo pamoja na
kukamata mali nyingine ambayo bado haijapatikana.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya pia
linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha
madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani.
Aidha kumekuwa na tukio 01 la ajali ya kifo kama ifuatavyo:-
AJALI YA KIFO.
Mnamo
tarehe 08.09.2016 majira ya saa 07:00 asubuhi huko Mtaa wa Mama John, kata ya
Ruanda, tarafa ya Iyunga, Jiji na mkoa wa Mbeya. Gari lenye namba za usajili T.712
DDF aina ya Toyota Coaster ikiendeshwa na dereva SIKU JORDAN (40) mkazi wa Veta ilimgonga mpanda baiskeli mwanaume
asiyefahamika, mwenye umri wa miaka kati ya 23 hadi 25 na kusababisha kifo chake.
Chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari. Dereva amekamatwa, mwili wa marehemu
umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Upelelezi unaendelea.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa
Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa
wito kwa wafanyabiashara kuacha tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka kwa
njia zisizo halali kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kujikuta wananunua bidhaa
feki au mali za wizi na kujisababishia matatizo. Pia Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi
kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za
uhalifu na wahalifu. Aidha anaendelea kutoa wito kwa madereva na watumiaji wa
barabara kuwa makini hasa kwa kufuata na kuzingatia sheria na alama za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.
Imesainiwa
na:
[DHAHIRI A.
KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
