Mchezaji wa Simba Shiza
Kichuya akishangilia huku akiwa amebebwa na Laudit Mavugo mara baada ya
kuifungia timu yake ya Simba goli katika dakika ya 67 kwenye
kipindi cha pili cha mchezo wa ligi kuu ya Vodacom katika uwanja wa Uhuru
wakati Simba ilipocheza na timu ya Azam FC Jumamosi septemba 17, 2016jijini Dar es salaam ,
Katika mchezo huo Simba imetoka kifua mbele kwa kuibuka na ushindi wa
goli 1-0 dhidi ya Azam FC
Wachezaji hao Walishangilia goli
lao na kukimbilia mbele ya bango la picha ya mchezaji aliyekuwa kipenzi cha
mashabiki wa timu hiyo Marehemu Patrick Mafisango aliyepoteza maisha kwa ajali
ya gari jijini Dar es salaam na kusafirishwa nchini kwao DRC Congo, ambako
alipumzishwa katika nyumba yake ya milele akiwaachia majonzi makubwa
mashabiki wa Simba kutokana na umahiri wake katika kucheza mpira ambao
uliisaidia na kuipa mafanikio klabu hiyo.
Mchezaji wa Simba Laudit
Mavugo akishangilia na wenzake mbele ya picha ya Marehemu Patrick Mafisango
aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu hiyo kama kumbukumbu yake katika mchezo
uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru huku Simba ikiibuka na ushindi wa Goli
1-0 dhidi ya Azam FC.
Mchezaji Ibrahim Ajib wa Simba
akichuana vikali na Mchezaji Brce Kangwa wa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom uliozikutanisha timu za Simba ya Dar es salaam na Azam FC pia ya Dar
es salaam.
Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia
mchezo huo wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa Uhuru.
Mchezaji wa Simba Laudit Mavugo
akiwatoka mabeki wa timu ya Azam FC Shomari Kapombe na mbele na David Mwantika
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa Jumamosi septemba 17, 2016 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Simba Laudit Mavugo
akiondoka na mpira mbele ya mabeki wa timu ya Azam FC Shomari Kapombe
kulia na David Mwantika kushoto katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom uliochezwa leo kwenye uwanja wa Uhuru
Piga nipige ikiendelea wakati wa
mchezo huo.







0 Comments