
Na Mahmoud Ahmad ARUSHA
SERIKALI
wilaya ya Arusha, imewataka wazazi ambao wamewatelekeza watoto wao
mitaani kwa kushindwa kuwalea kuhakikisha wanawajibika kuwaondoa na
kuwarejesha majumbani na kuwapatia malezi bora,badala ya kuwaacha
waendelee kuishi kwenye mazingira magumu.
Hayo
yalielezwa na mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro,
alipokuwa akifungua mafunzo ya utambulisho wa mfumo wa manegmenti
ya kesi za watoto kwa wadau wa huduma ya ulinzi na usalama wa watoto
katika jiji la Arusha na wilaya ya Karatu.
Daqarro,
alisema katika jiji la Areusha kuna watoto waishio kwenye mazingira
magumu na hatarishi wapatao 18834,kutokana na wazazi kutokutimiza
wajibu wa kuwalea ,hivyo umefika wakati wazazi lazima wahakikishe
wanawaondoa watoto kwenye mazingira hayo hatarishi vinginevyo serikali
itawalazimisha.
''Serikali haitaki kuona watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na hatarishi huku wazazi wao wapo "'alisema Daqarro.
alisema
haiwezekani wazazi kuwaacha watoto wakihangaika na kutaabika mitaani
na kukosa haki zao za msingi zikiwemo elimu, afya,malazi ,lishe bora
na upendo, hivyo lazima wahakikishe wanawarejesha majumbani watoto wao.
Aidha,
aliupongeza mpango huo ambao umewezesha jiji la Arusha, kuweza
kusimamia huduma mbalimbali za watoto kwa kuwa wangelikuwa kwenye
hali mbaya kutokana na mazingira waliyokuwa wakiishi.
Ameutaja
mpango huo wa Pamoja Tuwalee umesaidia watoto kupata ulinzi ,usalama ,
afya na kuiwezeshja jamii kutoa mafunzona huduma kwa watoto waishio
kwenye mazingira hatarishi.
Aliwataka
mganga mkuu wa jiji la Arusha na Idara ya ustawi wa jamii, kuhakikisha
wanazingatia matumizi sahihgi ya mfumo huo ili kuepuka kufanya kazi
kwa mazoea na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha walengwa
kwa kutambua wahitaji.
Awali,
mkurugenzi wa shirika World Education ,Hindu Ally Mbogo, alisema
mpango huo wa Pamoja Tuwalee unafadhiliwa na shirika la misaada la
Marekani, USAID, umesaidia kuokoa maisha ya watoto waliopo kwenye
mazingira hatarishi.
Alisema
mpango huo kuwafikia watoto na kuwapatia huduma mbalimbali ikiwemo
kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa taifa wa Pamoja Twaweza Program, Liliani Badi
Manara, alisema awamu ya kwanza ya mradi huo inakamilika Novemba 2016
Aidha
awamu ya pili ya mradi huo wa miaka mitano unaofadhiliwa na shirika la
misaada la Marekani USAID, itatekelezwa na shirika la Pact Tanzania