Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga alipotembelea banda la upimaji afya katika Uwanja wa Taifa wakati wa Mechi ya Wabunge wa Simba na Yanga.
Waziri wa Habari Bw. Nape
Nnauye akiongozana na Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Bi. Grace
Michael kuelekea kwenye banda la Mfuko
huo ambalo liliendesha upimaji wa afya kwa wananchi wote waliofika uwanjani
hapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Bernard Konga akipokea cheti kutoka kwa Waziri Mkuu ambacho kinautambua mchango
wa Mfuko katika janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Mbunge wa Sengerema Bw. William
Ngeleja akipima uzito kabla ya mtanange kati ya wabunge wa Yanga na Simba.
Katibu Mkuu wa Wizara y Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Gabriel akipima kiwango cha sukari
katika banda la NHIF.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw. Nape Nnauye akipima uzito kabla ya mechi kuanza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mfuko huo.
..............................................................................................................
Na Grace Michael
WAZIRI Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima kwa kazi kubwa inayofanya ya kuwahudumiwa
wanachama wake lakini pia kuendesha shughuli za upimaji wa afya bure katika
maeneo mbalimbali.
Pamoja na pongezi hizo, ameutaka Mfuko huo
kuangalia namna ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi katika suala la upimaji wa
afya ili kila mmoja ajue hali ya afya yake.
“Kwanza niwapongeze tu kwa kazi kubwa
mnayoifanya hapa ya kutupima afya zetu...hakikisheni shughuli hizi zinafanyika
mahali pengi zaidi kwani kwa sasa kuna mwamko mkubwa sana wa wananchi kupima
afya zao, hata pale bungeni leteni huduma hizi wakati wa bunge ili waheshimiwa
wabunge nao wapate fursa hii,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
umekuwa msaada mkubwa katika usimamizi na utoaji wa huduma za matibabu kwa
wanachama wake pamoja na uboreshaji wa huduma za matibabu.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kutoa wito
kwa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu
wakati wowote wanapohitaji lakini pia kuhakikisha wanatumia fursa za upimaji wa
afya zinapokuwa katika maeneo yao.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Bw. Nape Nnauye akizungumzia zoezi la upimaji lililofanywa na NHIF
uwanjani hapo, alisema kuwa ni jambo zuri kwa kuwa mbali na watu kujua hali ya
afya zao lakini watapata elimu ya namna ya kujiunga na huduma za Mfuko.
Alitoa wito kwa vijana kuhakikisha wanajenga
tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujua hali zao kwa kuwa ndio nguvu
kazi inayotegemewa katika uzalishaji wa Taifa hili.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Bw. Bernard Konga alisema kuwa, Mfuko umeendesha zoezi hilo uwanjani hapo kwa
lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali hususan katika
kushughulikia tatizo la janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.







0 Comments