Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania
Septemba 21, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othman baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango
Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania
Septemba 21, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Dkt, Tulia
Ackson baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati
na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21,
2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza katika
uzinduzi Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya
Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha
Septemba 21, 2016.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika
uzinduzi Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya
Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha
Septemba 21, 2016.
Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia,
Bella Bird akizungumza katika uzinduzi Mpango Mkakati na Mradi wa
Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza katika uzinduzi
katika uzinduzi Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za
Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini
Kibaha Septemba 21, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othaman kukata utepe wakati alipozindua Mpango Mkakati na Mradi
wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania mjini Kibaha, Septemba
21, 2016.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Nchi
za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird kitabu cha Mradi wa
Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania baada ya kuuzindua mjini
Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed
Chande Othman na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Mpango Mkakati na
Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la jengo la Mahakama ya
Hakimu Mkazi Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Sptemba 21, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa Mpango Mkakati na Mradi wa
Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akiondoka baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo
la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya wilaya ya Kibaha
Septemba 21, 2016. Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande
Othman na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za
Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa
nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (kulia kwake)
na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) baada ya kuweka
jiwe la msingi la jengo la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya
wilaya ya Kibaha Septemba 21,2016. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na. Sheila Simba-MAELEZO
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 14 kwa taasisi za serikali
zinazomiliki viwanja bila kuviendeleza mkoani Pwani viwanja kuanza mara
moja hatua ya kuendeleza maeneo yao.
Aliyasema
hayo leo Kibaha Mkoani Pwani wakati alipokuwa akizundua uzinduzi mpango
mkakati (2015-20) na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama nchini.
Amezitaja
taasisi za umma zinazomiliki viwanja hivyo ni Wizara ya fedha, Njuweni
Institute, Chuo kikuu Huria, Shirika la umeme nchini (Tanesco) Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU).
“Taasisi
hizi ziandikie barua na waseme lini wataviendeleza viwanja hivi mpaka
mwezi wa sita 2018 na waanze mara moja ujenzi viwanja hivyo baada ya
hapo vitarudishwa kwa mkoa na tutawapa watu wengine”,alisema Majaliwa
Aidha,alisema
Waziri mkuu aliipongeza mahakama kwa mpango wake huo wa kuendeleza na
kujenga majengo ya mahakama nchini wenye lengo la kumsaidia mwananchi wa
kawaida kupata huduma za mahakama kwa urahisi.
Majaliwa
alisema kuwa mahakama nichini zinatakiwa kuzingatia kutenda haki kwa
watu wote bila kujali hali ya mtu,kijamii au kiuchumi na kutochelewesha
haki bila sababu za msingi.
Aliongeza
kuwa mahakama inapaswa kutoa fidia ipasavyo kwa watu walioathirika
kutokana na makosa ya watu wengine kwa mujibu wa sheria.
“lengo
la mhimili huu ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwapunguzia
umbali wanaotembea kufuata huduma na unalenga kupunguza muda wa mashauri
kukaa mahakamani”alisema Waziri Mkuu Majaliwa
Kwa
upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande alisema mpango
mkakati wa mahakama nchini ni dira na muelekeo wa kufikia lengo la kuwa
na karibu na wananchi na kutoa huduma za utoaji haki.
Ameeleza
kuwa mahakama imejipanga kufika malengo ya dira ya maendeleo 2025 ya
kufikisha nchi kwenye uchumi wa kati kwa kutekeleza uadilifu, usawa,
ushirikiano, weledi, uwajibikaji na uwazi.
Jaji
Mkuu Chande ametaja malengo waliojiwekea mahakama ni utawala
bora,uwajibikaji, usimamizi wa rasilimali, upatikanaji na utoaji wa haki
kwa wakati na kuimarisha imani ya jamii na ushirikishaji wa wadau
katika shughuli za mahakama.
“Tunachofanya
sasa ni kuboresha miundombinu ya mahakama mijini na vijijini, kuongeza
fursa ya upatikaji wa haki kwa makundi maalum ya wahitaji na kubadilisha
tawsira ya mahakama” alisema Jaji Mkuu
Jaji
Mkuu Othuman Chande,mahakama imefanikiwa ndani ya miaka 3 kufika lengo
la kuwa na asilimia 80 ya mashauri ukilinganisha na miaka 3 ya nyuma
wakati asilimia 80 ya mashauri yalikuwa ni yale ya miaka 5 na miaka 20.
Alieleza
kuwa kwa kipindi cha mwaka 2016 2017 wanamalengo ya kimkakati ya
kuondokana na mashauri yote yenye zaidi ya miezi mitatu hadi sita kwa
mahakama za mwanzo,wilaya na hakimu mkazi.
Naye
mwakilishi mkazi wa benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird alisema
wameikopesha serikali Tsh 141 Bilioni ili kusaidia katika kuboresha
huduma za mahakama kutokana na umuhimu wake katika kutoa haki kwa jamii
ya kitanzania.
0 Comments