Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na waandishi
wa habari Jijini Dar es Salaam mara
baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika
Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016 Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3 kwa 2.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
................................................................................................
Na
Raymond Mushumbusi- WHUSM.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Millioni moja kwa kila goli litakalofungwa na Serengeti Boys
katika mechi ya marudiano nchini Congo Brazaville.
Ametoa
ahadi hiyo wakati akiongea na kuwapongeza wachezaji hao mara baada ya
kumalizika kwa mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Congo Brazaville
uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
“Kwa
niaba ya Watanzania wote nawapongeza kwa mchezo mzuri mliouonesha na kuibuka na
ushindi lakini bado mnatakiwa kujituma kama mlivyofanya katika mechi hii na
naahidi kutekeleza ile ahadi yangu ya laki tano kwa kila goli na nitatoa tena
kwenu Millioni moja kwa kila goli mtakalofunga Congo Brazaville.”Alisema Mhe.
Waziri Nape.
Kwa
upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw. Bakari
Shime ameshukuru Waziri na Watanzania kwa ujumla kwa kujitokeza kwa
wingi kushuhudia mechi hiyo na watahakikisha wanapata ushindi katika mechi ya
marudiano kwani wameshayaona mapungufu yaliyojitokeza na watayafanyia kazi wachezaji
watakuwa tayari kuivaa tena Congo Brazavile.
Aidha
Nahodha wa Timu hiyo Bw. Issa Abdi
Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma
zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata
maagizo kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo
wa marudiano.
“Tunashukuru
sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu
tupate ushindi tukiwa ugenini ili tuweze
kufuzu” Aliongeza Nahodha Makame.
Timu
ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini
ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti
Boys) inayowania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika
(AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017 inatakiwa
kupata ushindi ili kujihakikishia kufuzu kwa fainali hizo.

0 Comments