Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na wachezaji wa
Serengeti Boys katika hafla fupi ya kuwakabidhi Shilingi Milioni Tano kama
motisha kabla ya mechi ya leo dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika
Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania(TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa maelezo juu ya maaandalizi ya mechi
kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa
Taifa Septemba 18,2016.
Kocha wa Serengeti Boys Bw. Bw.Bakari Shime akimshukuru Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) kwa
kuwapa motisha wachezaji kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na
Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Nahodha wa Serengeti Boys Bw. Issa Abdi
Makame akiahidi kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye (Hayupo Pichani) kuibuka na ushindi dhidi ya Congo-Brazaville katika
mechi itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akimkabidhi Millioni tano Nahodha wa Serengeti Boys Bw.
Issa Abdi Makame kama motisha kabla ya kabla ya mechi ya leo dhidi ya
Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys
wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville
itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
(Picha zote na
Raymond Mushumbusi WHUSM)
............................................................................................
Na
Shamimu Nyaki- WHUSM.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa kiasi cha
shilingi million tano kwa timu ya Serengeti Boys kama motisha katika mchezo wao
dhidi ya Congo Brazivile utakayochezwa leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar
es Salaam.
Akikabidhi
pesa hizo leo Jijini Dar es Salaam Mhe.
Waziri Nape amewataka wachezaji hao kujituma zaidi katika mechi hiyo ili wapate
ushindi utakaowawezesha kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika kwa
vijana chini ya miaka 17 .
“Watanzania
wote tupo pamoja na nyie endeleeni
kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya pili, Sisi kama Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia heri
ili mlete heshima kwa Taifa.”Alisema Mhe. Nape.
Kwa
upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw.Bakari
Shime amemuhakikishia Waziri na Watanzania kwa ujumla kuwa mechi ya leo
watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo
tayari kuivaa Congo Brazavile.
Aidha
Nahodha wa Timu hiyo Bw. Issa Abdi
Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma
zaidi kwa kushirikiana na wenzake na
kufuata maagizo kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata ushindi.
“Tunashukuru
sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu
tupate ushindi ili tusonge mbele zaidi ”
Aliongeza Nahodha Makame.
Timu hiyo ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys)
inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana
yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.







0 Comments