Mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom kati ya Stand United iliyokuwa mwenyeji wa Yanga, umemalizika kwa
mabingwa watetezi wa VPL, Yanga kukubali kichapo kutoka kwa chama la wana,
Stand United.
Mchezo huo
umemalizika kwa Yanga kufungwa goli moja kwa bila, goli likifungwa na Pastory
Athanas katika dakika ya 58 baada ya mabeki wa Yanga kuchanganyana na Athanas
kutumia nafasi hiyo kwenda kufunga goli lililodumu hadi mchezo unamalizika.
Kwa matokeo hayo, Stand
United imefikisha alama 12 ikiwa nafasi ya tatu ya msimamo wa VPL na Yanga
ikisalia na alama 10.
Kipigo hicho kwa
Yanga kinakuja ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kukutana na watani zao wa jadi
Simba, mchezo unaotaraji kupigwa Jumamosi ya Oktoba mosi katika dimba la taifa.

0 Comments