Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akikabidhi hundi
ya kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini
Mhe, Hussein
Bashe (kulia) Kwa ajili ya kuwezesha vijana wajasiriamali waishio
katika kata 10 zilizoko ndani ya Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora
kupata mikopo yenye riba nafuu itakayosaidia kutatua changamoto za ajira
kwa vijana. Programu hii inaendeshwa kwa ushirika
kati ya Airtel
Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” na asasi
iliyoundwa kimikakati na Mbunge huyo ya Nzega Urban Trust Fund ili
kumaliza
tatizo la umasikini wa kipato katika jimbo la Nzega Mjini.
Mbunge
wa jimbo la Nzega Mjini Mhe, Hussein Bashe (kushoto) akiongea na
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso (kulia) wakati
alipotembelea ofisi za Airtel
juu ya program ya WanaNzengo Airtel FURSA inayowawezesha vijana
wajasiriamali waishio katika kata 10 zilizoko ndani ya Jimbo la Nzega
Mjini mkoani Tabora kupata mikopo yenye riba nafuu itakayosaidia kutatua
changamoto za ajira kwa vijana.
Programu
hii inaendeshwa kwa ushirika kati ya Airtel Tanzania kupitia mpango
wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” na asasi iliyoundwa kimikakati na
Mbunge huyo ya Nzega Urban
Trust Fund ili kumaliza tatizo la umasikini wa kipato katika jimbo la
Nzega Mjini.
..........................................................................................................................
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalum wa kusaidia jamii wa
Airtel FURSA Tunakuwezesha leo imekabidhi hundi ya shilingi
milioni 20 kwa Mbunge wa Nzega ikiwa ni harakari za kukamilisha dhamira
yake ya kushirikiana na jamii katika kuinua vijana sehemu mbalimbali
hapa nchini.
Akikabidhi hundi
hiyo Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sunil Colasa alisema “Airtel
imejipanga kwa kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na mradi wa
Airtel FURSA kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao
waliyoipanga kwa kupunguza changamoto walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa
ajira na mtaji ili watimize malengo yao katika biashara”
“Tunaamini
kupitia ushirika wetu na Mbuge Nzega Mh, Hussen Bashe mfuko wa Nzega
Trust Fund utasaidia wananchi ndani ya vijiji 21 katika jimbo hilo
ambapo malengo yetu ni kufanya mradi huu kuwa endelevu hata
kwa majimbo mengine nchini” alisema Bw, Colasa
kwa upande wake
Mbunge wa Nzega Mjini Mh, Hussen Bashe aliishukuru Airtel nakuahidi
kusimamia mradi huo wa ukopeshaji kwa ajili ya kuweza kuinua vipato vya
wananchi wa Nzega kama ilivyokusudiwa
“Nitoa wito kwa wananchi wote wenye malengo ya kujiendeleza kujitoza na kujisajili katia Mfuko wetu wa
Nzega Trust Fund niliouanzisha kwaajili ya kuhakikisha tunaungana
na wadau wenye nia ya kusaidia jamii kama Airtel FURSA ili kupunguza
changamoto za maendeleo kwa wananchni hasa kwa wanaokosa mitaji ya
kuendesha Miradi yao mbalimbali”
“Airtel tayari
wamezikabidhi pesa hizi kwangu ambazo tutazikopesha kwenu kwa Riba ya
1.5% pale unaporejesha na faida inayopatikana bado itaendelea kuwasaidia
vijana wengine watakaotaka kukopa” Alieleza Mh Bashe
Mradi wa Airtel
Fursa umeanzishwa Mei mwaka uliopita na tayari umewafikia vijana zaidi
ya Elfu tano kutoka katika mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na vijana
zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea
kazi mbalimbali
Programu hii
kati ya Airtel na Nzega Trust Fund chini ya Mbunge wa Jimbo la Nzega
Mjini Mhe. Hussein Bashe, itawawezesha zaidi ya wajasiriamali 350
kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money. Mikopo
hii itatolewa kwa kikundi kilichoundwa na vijana watano ambao watapewa
mtaji kati ya shilingi Shs.100,000 hadi 1,000,000 kulingana na
mahitaji yao. Sambamba na mikopo ya WanaNzengo Airtel FURSA vikundi vya
wajasirilamali vitaendelea kupewa mafunzo ya
ujasiriamali ikiwa ni pamoja na namna ya kuendesha vikundi pamoja na
jinsi ya kutafuta soko.


0 Comments