
Mgonjwa
ambaye majina yake hayafahamiki amelazwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali na kujeruhiwa
sehemu ya kichwani.
Mgonjwa
huyu alifikishwa katika hospitali hiyo tarehe 25-09-2016 akitokea
Hospitali ya Vijibweni jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa fomu namba
tatu ya polisi (PF3), mtu aliyegonga alikimbia.
Mgonjwa
huyo hawezi kuzungumza na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali
hiyo. Mgonjwa amelazwa Kibasila, wodi namba tisa. Endapo kuna mtu au
ndugu anamfahamu mgonjwa huyu afike Muhimbili ofisi ya Ustawi wa Jamii
au Ofisi ya Uhusiano Muhimbili.
0 Comments